MVUTANO wa kisheria kati ya Umoja wa Ulaya (EU) na kampuni ya kutengeneza chanjo ya Corona, AstraZeneca, umefikia suluhu na sasa pande mbili hizo zitaendelea kushirikiana katika mapambano dhidi ya ugonjwa huo.
Awali, EU iliikalia kooni AstraZeneca ikidai kampuni hiyo ilisambaza idadi ndogo ya chanjo, tofauti na makubaliano, na kesi hiyo ilitarajiwa kufikishwa kwenye mahakama za jijini Brussels, Ubelgiji.
Baada ya pande mbili hizo kuelewana, sasa AstraZeneca itasambaza chanjo milioni 200, idadi ambayo iliahidi kwenye mkataba wa Machi, mwaka huu.
Juu ya zoezi la chanjo, EU ilitoa taarifa yake wiki hii ikieleza kuwa asilimia 70 ya raia wa nchi wanachama wamechanjwa awamu ya pili.