27.1 C
Dar es Salaam
Thursday, January 2, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Etihad yazoa tuzo Uingereza

Edward Plaisted
Edward Plaisted

LONDON, UINGEREZA

SHIRIKA la Ndege la Etihad, limetunukiwa tuzo tatu za ubora wa madaraja, huduma za vyakula na kwenye malazi mjini hapa juzi.

Tuzo hizo za kimataifa zilizotolewa na taasisi ya Skytrax Worldairline Awards, uhusisha mashirika ya ndege yanayofanya vizuri katika sekta ya usafiri wa anga katika mataifa 100 duniani.

Katika taarifa yake, shirika hilo lilisema: “Mwaka 2014 tuliingia kwenye ushindani kwa kutambulisha ndege zetu za abiria, Airbus A380 na Boing 787 Dreamliner. Jambo hili limeonyesha dhamira yetu ya kuwa wa kwanza katika kutoa huduma ya kisasa na uvumbuzi.

“Tunafarijika kwa ushindi huu unaotokana na uwekezaji wa huduma bora kwa wateja wetu duniani, na hivyo kuzidi kuwa wa kwanza kwa ubora katika maeneo yote.”

Mwenyekiti wa Skytrax, Edward Plaisted, alisema “Shirika la Ndege la Etihad limekuwa likiimarika na kuwa bora zaidi katika usafiri wa anga kwa kuendana na mabadiliko ya teknolojia ya kisasa katika utoaji wa huduma zake.

“Kwa mara nyingine tena shirika hili limenyakua tuzo tatu muhimu kwa kupigiwa kura na mamilioni ya wasafiri duniani kote, ambapo ni dhahiri lilistahili kuwa mshindi kutokana na kutoa huduma za kiwango cha juu.”

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles