24.4 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 23, 2024

Contact us: [email protected]

Zingatia haya ili kuwa salama na fedha zako

Online transaction

NA FARAJA MASINDE,

MARA kwa mara TCRA imekuwa ikisisitiza juu ya hatari ya utapeli wa fedha ambao umekuwa ukifanyika kwenye benki au simu za mkononi kwa njia ya kufanya malipo.

Ili kuwa salama na fedha zako itakuwa busara zaidi ukisoma na kuzingatia dondoo hizi kuliko vile ambavyo ungepuuza na kuendelea kuamini namba za siri (password) zako kwa kuwa wezi nao wanajaribu kwenda na kasi ya teknolojia.

Hakikisha unaweka neno la siri (password)

Hii ni hatua muhimu sana kwenye kuweka fedha zako salama zinapokuwa benki au kwenye simu kupitia Apps za usalama.

Hii itakusaidia kutokana kwamba kwani iwapo mtu hafahamu namba ya siri ya simu yako hata kama anajua neno la siri ya akaunti zako za fedha haweza kufanya chochote.

Ondoa jumbe zote za miamala kwenye simu

Hili liko wazi kuwa pindi unapoacha ujumbe unaoanyesha kiwango kilichobakia kwenye akaunti yako ya benki au simu inaweza kumrahisishia mwizi kujua unakiwango gani na hivyo kumhamasisha, hasa pale unaposhindwa kuwa makini na simu yako.

Ukipoteza simu ripoti

Ni jambo la busara ukitoa taarifa pindi unapokuwa umepoteza simu, vuta picha kama huna namba ya siri kwenye simu yako iliyopotea na inafedha ndani yake.

Unaweza kuwasiliana na mtandao wako unaotumia au hata benki husika juu ya kuthibiti akaunti yako.

Faida ya hili ni kuwa mtu hatakuwa na uwezo wa kutoa fedha zako zilizokwenye akaunti kwa maana ya kukuibia, hata kama atakuwa anafahamu namba zako za siri za akauti.

Pia huduma hii inamzuia mtu yeyote mwenye nia ovu na laini yako.

Usimwamini kila mtu

Hii inamaana kuwa hata kama mtu akikupigia kwa simu na kujitambulisha kama ni mtoa huduma kutoka mtandao wa simu unaotumia au benki unayotumia na akataka umpatie taarifa zako muhimu kama vile PIN/Password ya akaunti yako usikubali kabisa.

Acha kutuma fedha unapoombwa kwa ‘SMS’

Watu wengi wenye malengo mabaya na wewe hutumia mwanya wa ukaribu ulionao na mtu fulani kujitapatia fedha kirahisi.

Kwani ni mara nyingi inatokea mtu wako wa karibu kuhitaji msaada wako wa kifedha, hivyo ni vyema ukachukua jukumu la kumpigia simu kwanza ili kuweza kujiridhisha ikiwa ndiyo yeye hasa anayeomba.

Nifuate kwenye 0653045474

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles