28.2 C
Dar es Salaam
Thursday, November 21, 2024

Contact us: [email protected]

Etihad yazindua jumba la kupumzikia abiria

Etihad_AirwaysMELBOURNE, AUSTRALIA

SHIRIKA la Ndege la Etihad juzi lilifungua rasmi jumba lao jipya la kifahari la kupumzikia wageni kwenye Uwanja wa Ndege wa Melbourne, nchini hapa.

Jumba hilo lililo katika eneo lenye nuru ya asili na vioo kuanzia sakafuni hadi katika dari, linawapatia wageni mtindo pekee, mazingira tulivu kabla ya safari likiwa na mgahawa na viburudisho na huduma karibu zote stahili ikiwamo mtandao wa Wi-Fi wenye kasi.

Likiwa na ukubwa wa mita za mraba 800 na uwezo wa kukalisha na hadi vyumba vya kupumzikia wageni 133, ni eneo kubwa zaidi la kupumzikia abiria la shirika hilo nje ya Abu Dhabi, Muungano wa Falme za Kiarabu (UAE).

Makamu Mkuu wa Rais wa Masoko wa Etihad, Shane O’Hare, ambaye alikata utepe wakati wa sherehe ya ufunguzi pamoja na Ofisa Mtendaji Mkuu wa shirika hilo mjini Melbourne, Lyell Strambi alisema:

“Nyumba mpya ya kupumzika wageni ya kifahari iliyoko Uwanja wa Ndege wa Melbourne ni daraja la peke yake. Ni makazi ya kupumzikia ya uwanja wa ndege kama ambavyo inajulikana, yaliyoboreshwa zaidi.”

“Ikiunganisha mgahawa bora wa chakula na baa ya vinywaji, nyumba hii ni maonyesho ya ubunifu na umakini, ambao wageni watafurahia kiwango cha juu cha utulivu na starehe, inayokamilishwa na ukarimu wetu wa kiwango cha kimataifa, ubunifu katika mapishi na teknolojia ya kiwango cha juu ya vinywaji.”

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles