27.2 C
Dar es Salaam
Friday, November 29, 2024

Contact us: [email protected]

Ethiopia yatambua rasmi Baraza Kuu la Waislamu

Addis Ababa, Ethiopia

Ethiopia yatambua rasmi Baraza Kuu la Waislamu baada ya juhudi za miaka 60.

Baada ya juhudi za miaka 60 hatimaye Baraza Kuu la Waislamu nchini Ethiopia limetambuliwa rasmi na Serikali ya Addis Ababa, suala ambalo limetajwa na wachambuzi wa mambo kuwa ni mafanikio ya kihistoria kwa wafuasi wa dini hiyo nchini Ethiopia.

Ofisi ya Waziri Mkuu wa Ethiopia, Abiy Ahmed, imetangaza kuwa, Baraza la Mawaziri limepasisha kwa sauti moja sheria inayotambua rasmi Baraza Kuu la Waislamu linalosimamia masuala ya jamii ya Waislamu nchini.

Uamuzi huo umechukuliwa kujibu matakwa ya Waislamu wa Ethiopia ya kutambuliwa kisheria taasisi ya kidini inayosimamia masuala yao ya kimaisha na kudhamini haki zao za kuwa na mahusiano na taasisi mbalimbali za kidini na zisizo za kidini.

Baada ya kutambuliwa rasmi, sasa Baraza Kuu la Waislamu nchini Ethiopia linakuwa taasisi ya kidini yenye mamlaka kamili inayoweza kutunga sheria zinazohusiana na masuala ya Waislamu na kuanzisha taasisi zake mahususi.

Waislamu wa Ethiopia

Mwezi Mei mwaka jana, Waislamu wa Ethiopia walikubaliana kuunda kamati ya muda ya maulama inayoongozwa na Mufti Mkuu wa nchi hiyo Haji Omar Idris kwa ajili ya kusimamia masuala ya Waislamu hadi itakapoundwa taasisi mpya ya Waislamu nchini humo. Waislamu hao walitaka kuundwa taasisi inayowakisha wafuasi wote wa dini hiyo na kudhamini uhuru wao ambayo haitatumiwa kwa malengo ya serikali.

Kutambuliwa rasmi Baraza Kuu la Waislamu nchini Ethiopia kumetajwa kuwa ni mafanikio makubwa ya kihistoria baada ya juhudi za miaka 60 za wafuasi wa dini hiyo za kutambuliwa kisheria tasisi inayosimamia masuala yao ya ndani na nje kama lilivyo Kanisa la Kiorthodoksi la Ethiopia.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles