25.9 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 1, 2021

Virusi vya Corona vinasambaa kabla mwathirika kutambua

Wuhan, China

Virusi vipya ya Corona ambavyo vimesambaa kwa watu karibia 2000 vinaambukiza wakati wa kuatamia mayai na dalili zinakuwa bado hazijaanza kujitokeza na kufanya iwe vigumu kudhibitika, wamesema maOfisa wa China.

Baadhi ya watu 56 wameaga dunia kwasababu ya virusi hivyo. Waziri wa Afya Ma Xiaowei aliwaambia wanahabari kwamba uwezo wa virusi hivyo kusambaa na unaonekana kuongezeka.

Baadhi ya miji ya China imepiga marufuku kabisa usafiri wa sehemu moja hadi nyingine.

Mji wa Wuhan uliopo Hubei, chanzo cha mlipuko wa virusi hivyo kwa sasa umefungiwa kabisa.

Maambukizi yako katika kiwango ambacho ni vigumu kudhibitika”, alisema Ma Xiaowei.

Maofisa wameahidi kuongeza juhudi maradufu za kudhibiti virusi hivyo na kutangaza kwamba biashara ya kuuza wanyama wote wa porini itapigwa marufuku kuanzia jana Jumapili.

Virusi hivyo vinaaminika kwamba vimetokana na wanyama na vimesambaa kwa haraka kati ya wanadamu.

Kipindi cha kuatamia mayai wakati ambao mtu ameambukizwa virusi lakini hakuna dalili zozote zinazojitokeza ni kati ya siku 1 hadi 14, maofisa wanaamini hivyo.

Bila ya kujitokeza kwa dalili mtu hawezi kufahamu ikiwa ameambukizwa virusi vya Corona lakini pia vinaweza kusambaa kwa wakati huo huo.

Katika barabara zinazoelekea mji wa Nanyang, watu wanakaguliwa. Yeyote ambaye ni mgonjwa haruhusiwi kuingia kwenye mji huo. Magari yenye namba zi miji mingine pia yanafuatiliwa kwa karibu.

Ndani ya mji huo, hoteli hazikubali wasafiri kutoka mji wa Hudei chimbuko la virusi vya Corona

Baadhi ya miji na vijiji haviruhusu mtu mwengine yeyote kuingia isipokuwa wenyeji pekee.

Maofisa kote nchini humo wanachukua hatua kali na kwa haraka ili kupunguza usambaaji wa virusi hivyo vinavyosababisha kifo.

Sophie, kutoka Uingereza yuko mjini Wuhan. Ameliambia shirika la BBC: “Tumekwama. Tumekuwa tu ndani ya nyumba kwa siku nne. Tulifahamu kuhusu virusi vya Corona Desemba 31. Na hali inaendelea kuwa mbaya kila uchao.

“Inatia hofu, tumesikia kwamba virusi hivi vinaweza kuwa ndani ya mwili kwa wiki mbili bila ya mtu kuonesha dalili zozote za kuugua. Kwa sasa tunafuatiliwa kwa karibu na familia zetu zimeingiwa na hofu,”  alisema.

Taxi hazipatikani barabarani na kwa sasa madereza wa kujitolea wanapeleka watu katika hospitali zilizojaa wagonjwa.

“Hakuna magari kwa hiyo tumejitolea kupeleka watu wenye uhitaji hospitalini na kuwarejesha, na baadaye tutapata kinga dhidi ya maambukizi bila malipo, ” Yin Yu aliliambia shirika la habari la AFP.

“Tuko salama. Lazima kuwe na mtu wa kufanya haya. Sisi tumetoka Wuhan, na pia nyinyi wanahabari muko hapa kutusaidia, raia wetu pia wanastahili kujitokeza kusaidia. Hili ni jukumu letu, ” dereva mwengine, Zhang Lin, alisema.

Virusi hivi vinasababisha matatizo ya kupumua. Dalili zake zinasemekana kuwa homa, kikohozi kikavu kisha baada ya wiki moja, mwathirika anakuwa na matatizo ya kupumua na kuhitaji matibabu kwa haraka.

Virusi hivyo vipya vinafananishwa na vile vya Sars, ambavyo vilisababisha vifo vya mamia ya watu 2003.

Hadi kufikia sasa, bado hakuna tiba maalum au chanjo dhidi ya virusi hivi.

Na kufikia Jumamosi, nchini Uchina kulikuwa na visa 1975 vilivyothibitishwa vya ugonjwa huo huku visa 2,684 zaidi vikishukiwa kuwa ni virusi hivyo, kulingana na Tume ya Taifa ya Afya ya Uchina.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,522FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles