24.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 23, 2024

Contact us: [email protected]

Erick Kabendera aomba kwenda kuzika

NA KULWA MZEE, DAR ES SALAAM

MWANDISHI wa Habari za uchunguzi,  Erick Kabendera , anayekabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi aomba ruhusa ya mahakama kwenda kuaga na kumzika mama yake mzazi huku Jamhuri wakipinga vikali.

Maombi ya Kabendera yaliwasilishwa jana katika Mahakama ya Hàkimu Mkazi Kisutu mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Janeth Mtega kupitia wakili wake, Jebra Kambole.

” Mheshimiwa hakimu mshtakiwa alifiwa na mama yake mzazi Desemba 31 mwaka huu, , tunamaombi madogo muhimu, tunaomba mahakama imruhusu mshtakiwa kwenda kuzika Bukoba ama kutoa heshima za mwisho kwa mama yake.”

Mwili wa mama wa mshtakiwa utaagwa katika Kanisa Katoliki Chang’ombe saa sita mchana hivyo tunaomba aruhusiwe chini ya ulinzi afike kutoa heshima za mwisho.

“Kutoa heshima za mwisho ni haki yake kikatiba na kuruhusiwa kwake hakuwezi kuathiri kitu chochote kwa upande wa Jamhuri, kumnyima ni kumpa adhabu kubwa na ya kinyama, mama mzazi ni mmoja, anazikwa mara moja, anaagwa mara moja …ni muhimu kuhudhuria tukio hili la kibinadamu,”alidai Jebra.

Akijibu Wakili wa Serikali Mwandamizi, Wankyo Simon alidai kwanza Jamhuri inatoa pole nyingi kwa msiba huo lakini wanasipinga hoja hizo sababu mahakama haina mamlaka ya kutoa amri hiyo.

Alidai mahakama imefungwa mikono na Mkurugenzi wa Mashtaka hajatoa kibali cha kuruhusu shauri hilo la uhujumu uchumi kusikilizwa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Wankyo aliomba maombi hayo yatupwe kwa sababu yamekuja kabla ya wakati wake lakini aliendelea kusisitiza pole nyingi kwa Erick kutokana na msiba mzito uliomkuta.Mahakama imeahirisha kesi hiyo itatoa uamuzi saa tisa kasorobo alasiri.

Kabendera anakabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi yenye mashtaka matatu likiwemo la utakatishaji wa zaidi ya Sh milioni 173.

Katika shtaka la kwanza ilidaiwa kuwa katika kipindi hicho, Kabendera alijihusisha  na mtandao wa kihalifu kwa kutoa msaada kwa genge la uhalifu kwa nia ya kujipatia faida.

Shtaka la pili ilidaiwa kuwa katika kipindi hicho,bila ya sababu,alikwepa kodi ya sh. 173,247,047.02 ambayo ilitakiwa ilipwe Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

Katika shtaka la tatu, kabendera anadaiwa kutakaisha Sh 173,247047.02 huku akijua fedha hizo ni mazalia ya kosa la kujihusisha na genge la uhalifu na utakatishaji fedha.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles