23.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 16, 2024

Contact us: [email protected]

EL-HADJI DIOUF ALISHINDWA KUZIMA UFALME WA GERRARD LIVERPOOL

NA BADI MCHOMOLO


el-hadji-dioufKATIKA wachezaji ambao wamekaa kwa muda mrefu katika klabu ya Liverpool, Steven Gerrard yupo katika orodha hiyo kwa kuwa aliweza kuitumikia klabu hiyo kwa miaka 18.

Alianza kucheza soka ndani ya klabu hiyo akiwa na umri wa miaka18 na akaitumikia kwa miaka 18 hadi mwaka 2015 alipoamua kuondoka huku mashabiki wa klabu hiyo bado wakiendelea kuhitaji msaada wake.

Siku zote nchini England ni ngumu kukupa ufalme katika soka kama utakuwa sio mchezaji wa taifa hilo, unaweza kupewa heshima yako kama utafanya makubwa zaidi ambayo yatakuwa hayafichiki machoni mwa mashabiki ulimwenguni.

Gerrard alipewa heshima ndani ya klabu hiyo kutokana na mchango wake kuwa mkubwa, pamoja na kutoa mchango ndani ya kikosi cha timu ya taifa nchini humo huku akiwa ni nahodha.

Alikuwa na uwezo mkubwa wa kucheza katika duara (kiungo), hivyo alionekana kama hana mpinzani ndani ya kikosi cha Liverpool hata timu ya taifa kwa ujumla. Lakini kila kitu kina mwanzo na mwisho wake.

Mbali na kufanya yote hayo ni kwamba England imekuwa ikitupiwa lawama kwa ubaguzi hasa kwa watu weusi, kwamba unaweza ukawa na uwezo mkubwa wa kucheza soka lakini ikawa ngumu kupewa heshima kubwa kutokana na rangi hasa kwa watu weusi, lakini uwezo huo ukiwa kwa raia wa nchini humo basi atakuwa mfalme.

Hakuna ambaye alikuwa hakumbuki uwezo wa nyota wa zamani wa timu ya taifa ya Senegal, El-Hadji Diouf, ambaye kutokana na uwezo wake alifanikiwa kupata nafasi ya kuitumikia klabu ya Liverpool ya nchini England, Sunderland, na nyingine nyingi.

Diouf alipata nafasi kubwa katika klabu ya Liverpool mara baada ya kuonesha moto wake katika michuano ya Kombe la dunia 2002 ambapo aliipeleka Senegal katika hatua ya robo fainali, ambapo hali hiyo ilimfanya mchezaji huyo kujiona bora zaidi.

Siku zote mafahali wawili hawakai zizi moja, hivyo ndivyo ilivyotokea kwa nyota huyo baada ya kukutana na Gerrard ambele alikuwa anapewa heshima yake ndani ya Liverpool, hivyo na Diof naye alikuwa na lengo la kupindua ufalme huo kitu ambacho kilikuwa kigumu kwa kuwa kama unavyojua England wanapenda cha kwao.

Diof alijaribu kutengeneza bifu dhidi ya nahodha wake, ambapo alimuanika kwa kusema kuwa mchezaji huyo ni mbaguzi hasa kwa wachezaji wenye rangi nyeusi, mbinafsi, pamoja na wivu wa maendeleo ya wachezaji wenzake.

Diof alicheza Liverpool kuanzia mwaka 2002 hadi 2005, ambapo alimkuta Garrard na kumuacha ambaye alianza tangu mwaka 1998 hadi 2015, lakini baada ya Diof kujiunga na klabu ya Bolton, Gerrard alisema kuwa hakuwa na urafiki na mchezaji huyo.

Kila mmoja alikuwa anaongea kivyake kwa kumponda mwenzake katika historia ya vitabu vyao. Wiki iliopita Gerrard alitangaza kustaafu soka, wakati Diof alitangaza mwaka jana, lakini baada ya Gerrard kutundika daruga, Diof alijitokeza katika kituo cha televishini nchini Ufaransa na kuanza kumshambulia mchezaji huyo.

“Wakati najiunga na Liverpool nilikuwa kwenye kiwango cha hali ya juu najua kwamba Gerrard kwa kipindi kile alikuwa anaamini kuwa naweza kuua kiwango chake hivyo baada ya kujua kwamba natua pale basi akaanza kuwa na wivu na mimi.

“Halikuwa hataki kuona mafanikio yangu hivyo alikuwa na wivu hasa kwa sisi watu weusi ambao tunafanya vizuri, nilikuwa katika historia ya wachezaji 100 ambao aliwataja nyota wa soka ulimwenguni Pele, lakini Garrard hakuepo katika orodha hiyo, hivyo wivu ulimzidi kutokana na mafanikio yangu.

“Naweza kusema sio kwa upande wangu tu, lakini ninaamini hata Mario Balotelli ni mchezaji mwenye uwezo mkubwa lakini ndani ya Liverpool alionekana kuwa hana thamani kutokana na wivu, ubinafsi wa Garrard kwa watu weusi.

“Ukweli utabaki pale pale kwamba nilikuwa kwenye ubora zaidi yake kwa kuwa niliweza kuipeleka Senegal katika robo fainali ya michuano ya Kombhe la dunia 2002, lakini yeye aliweza kufanya hivyo kwa England?

“Ninamuheshimu Garrard kwa kuwa alikuwa mchezaji, lakini yeye hawaheshimu wenzake, lakini kwa upande mwingine siwezi kusema alikuwa bora Liverpool, ila wapo ambao walikuwa bora zaidi yake,” alisema Diof

Bifu hilo linaonekana kuwa kubwa siku hadi siku, kwa kuwa kwenye baadhi ya vitabu vya historia ya Garrard ameonesha wazi kuwa alikuwa hamkubali Diof na Diof naye ameweka wazi kuwa mchezaji huyo alikuwa na wivu wa maendeleo kwa watu weusi. Ni wazi kwamba nyota hao kama watafanikiwa kuja kuwa makocha basi tutaona ushindani wa hali ya juu wakija kukutana.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles