24.7 C
Dar es Salaam
Saturday, April 13, 2024

Contact us: [email protected]

Efm yamzawadia pikipiki mjamzito

EFM SEBBONA ASIFIWE GEORGE

WAKAZI wawili wa Wilaya ya Temeke, Philipina Mshanga ambaye ni mjamzito na Salehe Maga, wameibuka washindi wa pikipiki mbili aina ya Boxer katika shindano la Shikandika lililoandaliwa na redio ya Efm.

Shindano hilo lilifanyika juzi huko Mbagala ambapo lilianza na washiriki 15 na wawili hao wakaibuka washindi.

Meneja Mkuu wa Mawasiliano wa kituo hicho, Denis Ssebo, alisema washindi hao walipatikana baada ya mchuano mkali wa kushika glasi ya maji kwa mkono mmoja na mguu mmoja ukiwa umenyanyuka juu.

“Tumeanza na Wilaya ya Temeke, tutafanya tena shindano hili katika wilaya ya Kinondoni, Ilala, Bagamoyo na Kibaha na washindi wote watajishindia pikipiki na mwisho wa mchuano washindi wengine wawili watajishindia magari mawili ya biashara aina ya Suzuki carry,” alieleza Ssebo.

Awali Efm waliwatangaza watangazaji waliojiunga na redio hiyo ambao ni Paul James, Gerald Hando na Abel Onesmo, waliokuwa Clouds FM. Efm redio hufanya shindano hili kwa lengo la kuwawezesha wasikilizaji wake kuongeza na kukuza kipato chao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles