26.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, May 21, 2024

Contact us: [email protected]

EFM yakabidhi gari, Kajala awapoza walioshindwa

Kajala-Masanja-akiwa-katika-poziNA ASIFIWE GEORGE
MKAZI wa Ilala, Stela Robert (26) na Gabriel Geoffrey (36) wa Temeke wameibuka washindi wa gari katika shindano la Shika Ndinga lililoandaliwa na Kituo cha Redio cha EFM cha jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Meck Sadick ndiye aliyewakabidhi funguo za magari yao maarufu kwa jina la Kirikuu lililofanyika katika viwanja vya Tanganyika Pekas Kawe huku akiwataka wasiofanikiwa kupata zawadi waendelee kujaribu bahati zao katika mashindano mengine yatakayoendeshwa na kituo hicho.
Naye Ofisa Uhusiano wa EFM, Lydia Moyo alisema shindano hilo lilikuwa na raundi nne ambapo washiriki walitakiwa washike kitu huku wakiwa wamesimama kwa miguu miwili, kisha wasimame kwa mguu mmoja na mwingine ukiwa umekunjwa kwa nyuma.
Alisema washiriki waliovumilia maumivu katika mizunguko hiyo minne walikuwa wawili ambao ndiyo walioibuka washindi ambapo mmoja kwa upande wa wanaume na mwingine kwa wanawake.
Hata hivyo, mwigizaji Kajala Masanja ‘Kajala’ aliwapoza washiriki wote walioshindwa kushinda gari kwa kuwapa pole yake ya Sh 10,000 kila mmoja.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles