28.7 C
Dar es Salaam
Friday, May 24, 2024

Contact us: [email protected]

Tunda Man: Shoo bora ni za wanyanyua vyuma

TUNDANA RHOBI CHACHA
NYOTA wa muziki wa Bongo Fleva nchini Tanzania, Khalid Ramadhani ‘Tunda Man’ amewaasa wasanii wenzake kufanya mazoezi kwa nguvu ili waweze kumudu maonyesho yao wawapo jukwaani.
“Wasanii wanatakiwa wafanye mazoezi yakiwemo‘push up’ na kunyanyua vitu vizito ili wajiweke sawa kiafya na kumudu shoo zao wawapo jukwaani,’’ alisema.
Tunda Man aliongeza kwamba wanaoshindwa kumudu jukwaani hawafanyi mazoezi ya kutosha na wanaofanya mazoezi hayo huwa na matokeo mazuri jukwaani.
“Hakuna uchawi jukwaani wasanii wanatakiwa wafanye mazoezi ya kutosha kama mimi napiga ‘push – up’, naruka kamba na nanyanyua vitu vizito kikiwemo chuma mazoezi ambayo yananisaidia sana kujiweka vizuri na kuweza kutawala jukwaa,’’ alimaliza Tunda Man.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles