Rais wa Ecuador Lenin Moreno, amesema mwasisi wa mtandao wa WikiLeaks Julian Assange alikiuka masharti ya hifadhi kwa kutumia ubalozi wa nchi hiyo jijini London kama kituo cha kufanya ujasusi wakati alipohifadhiwa humo kwa miaka saba.
Wakati wa utawala wa rais wa zamani wa Ecuador Rafael Correa, Assange alipatiwa hifadhi mnamo mwezi Agosti mwaka 2012, kutokana na kupokea vitisho kutoka taasisi za kiusalama za Marekani.
Lakini tarehe 11 mwezi huu, maafisa wa ubalozi waliwaruhusu polisi kuingia ndani ya jengo na kumkamata Assange baada ya kukiuka masharti ya dhamana ya Uingereza yanayohusishwa na ombi la Sweden la kutaka arejeshwe.
Polisi baadae walisema Assange ambaye ana uraia wa Austaralia alikamatwa kwa niaba ya mamlaka ya Marekani