24.5 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Droo ya pili ya M-Pawa yaibua washindi wengine

Mwandishi wetu – Dar s salaam

Benki ya CBA na Vodacom wamefanya droo yao ya pili ya promosheni ya Kukopa na kuwekeza na M-Pawa inayoendelea katika kusherehekea miaka mitano ya huduma hiyo ambapo washindi 40 walipata mara mbili ya akiba iliyopo kwenye akaunti zao ambayo ina kianzio cha kati ya shilingi 1,000 hadi shilingi laki mbili.

Droo hiyo ilifanyika jana Juni 20, katika ofisi za makao makuu ya benki hiyo jijini Dar es salaam, ambapo washindi hao wa droo ya pili walitangazwa mbele ya mwakilishi kutoka bodi ya michezo ya kubahatisha Jehud Ngolo, mtangazaji wa radio Efm na Mchekeshaji maarufu Silvery Mujuni ‘Mpoki’ akiwa na mtangazaji mwenzake Ummy Wenslaus maarufu ‘Dokii’ na wafanyakazi wa benki hiyo.

Washindi hao walichaguliwa kutoka makundi 3 ambayo ni kuweka akiba, kulipa mkopo mapema pamoja na Savings challenge na walipata mara mbili ya akiba iliyopo kwenye akaunti zao ambayo ina kianzio cha kati ya shilingi 1,000 hadi shilingi laki mbili huku wengine wenye zaidi ya shilingi laki mbili wakipata mara mbili ya kiasi hicho. Washindi wengine wa marejesho ya mkopo na Savings challenge wamezawadiwa simu pamoja na muda wa maongezi.

Akizungumza wakati wa uendeshaji wa droo hiyo, mwakilishi kutoka benki ya CBA Zainabu Mushi, alisema kuwa huduma ya M-Pawa inalenga zaidi kuwajali wateja wake na itaendelea kutoa zawadi mbalimbali katika kipindi cha pomosheni huku wakijidhatiti katika kuboresha huduma zao za kifedha na kujumuisha wateja wao.

“Tunawahimiza watumiaji wote wa huduma ya M-Pawa washiriki kwenye promosheni hii kwa kuweka akiba, kukopa na kurudisha mikopo yao mapema ili kujiweka kwenye nafasi ya kushinda pamoja na kuwahimiza watu wengine wasiotumia M-Pawa kuanza kutumia huduma hii,” amesema.

“Promosheni hii itaendelea kila wiki kwa muda wa wiki nne na mwisho wa promosheni hii kutakuwa na mshindi mkubwa atakayeibuka na zawadi ya pesa taslimu silingi milioni 15,” amesema.

Mmoja wa washindi hao, Elizabeth Mbogo, mjasiriamali kutoka mkoani Iringa aliyeshinda mara mbili ya akiba yake, alisema kuwa huduma ya M-Pawa inamsaidia sana kwenye kuhifadhi pesa zake huku ikimpa uhakika wa kukopa pesa pale anapohitaji.

Mshindi mwingine kutoka Kigoma, Tezeyo Abinal ambaye anajishughulisha na huduma za uwakala aliyeshinda mara mbili ya kiasi cha laki mbili kilichokuwa kwenye akiba yake alisema kuwa pesa hiyo itamsaidia kwenye kuongeza mtaji wa biashara yake na aliwahimiza watanzania wote kushiriki kwa kuanza kutumia huduma ya M-Pawa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles