23.7 C
Dar es Salaam
Saturday, September 23, 2023

Contact us: [email protected]

IGP: Tumeimarisha ulinzi nchi nzima

Bethsheba Wambura, Dar es Salaam

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, In­spekta Jenerali (IGP) Simon Sirro amesema, wameimarisha ulinzi nchi nzima.

Akizungumza na Mtanzania Digital leo Juni 21, IGP Sirro  amesema suala la kuwako kwa tetesi za sham­bulio katika eneo la Masaki jijini Dar es Salaam wanalifanyia kazi na ame­rudia kusisitiza jeshi hilo kuimarisha usalama si tu katika eneo hilo bali nchi nzima.

Katikati ya wiki hii ubalozi wa Marekani nchini ulitoa taarifa ya ku­wapo kwa uvumi wa shambulio katika eneo la Masaki, hususani katika hoteli wanazopenda kutembelea watalii na maduka yaliyopo eneo a ufukwe wa Bahari ya Hindi.

“Timu zetu zinafanyia kazi taarifa hizo, lakini siku zote tupo hivyo., ku­napokuwa na amani na utulivu siyo kwamba tumekaa au tumelala, kuna hizi timu zetu za ‘Intelligence’, watu wa operesheni na watu wa upele­lezi zimesambaa maeneo mbalimbali kuona kitu gani kipo.

“Ndiyo maana tukiona mtu asiye wa kawaida tunamkamata na kum­hoji, kwahiyo sisi tunafanya kazi yetu kama kawaida, kazi hiyo inafanyika maeneo yote yenye watu wengi na si Dar es Salaam pekee bali ni Tanzania nzima.

 “Ukizungumzia masuala ya ulinzi unazungumzia Tanzania nzima kwa hiyo haya tunafanyia kazi nchi nzima na si Dar es Salaam tu,” IGP Sirro amewaambia waandishi mara baada ya kumaliza mkutano na Maka­manda wa Polisi wa Mikoa na Maofisa wa Polisi uliokuwa ukizungumzia ukatili kwa wa watoto na wanawake uliokuwa ukifanyika Masaki, Dar es Saalaam .

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,699FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles