24.1 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Vipimo homa ya dengue sasa kutolewa bure

Ramadhan Hassan-Dodoma

Serikali imetoa kauli bungeni kuhusu mlipuko wa ugonjwa wa Dengue ambapo sasa imeamua kuwa vipimo kwa ajili ya homa hiyo vitaanza kutolewa bure kwenye vituo vya afya vya umma.

Hatua hiyo imekuja kufuatia hivi karibuni, mbunge wa Viti Maalum, Amina Molle (CCM) kutaka bungeni apewe majibu kuhusiana na ugonjwa huo ambapo alidai kwamba Serikali imekuwa kimya.

Leo Juni 21, mara baada ya kumalizika kipindi cha maswali na majibu, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Ummy Mwalimu alisimama na kutoa tamko la Serikali kuhusiana na ugonjwa huo ambapo amesema kuwa serikali imeagiza mashine kubwa sita kwa ajili ya kupulizia mbu wapevu ambazo  zinatarajiwa kufika mwishoni mwezi Julai.

“Kwa kuzingatia sheria hii Serikali ya awamu ya tano inayojali wananchi imeamua vipimo kwa ajili ya Homa ya Dengue vitatolewa bure kwenye vituo vya kutolea huduma za afya vya uuma,” amesema.

Amesema hatua ambazo Wizara imeshachukua mpaka sasa ni pamoja na kuangamiza mazalia ya Mbu wapevu na viluwiluwi ambapo imeishanunua kiasi cha lita 60,000 za viua vidudu kutoka kwenye kiwanda cha uzalishaji kilichopo Kibaha.

“Kati ya hizo lita 11,400 zimesambazwa kwenye Halmashauri 5 za Mkoa wa Dar es salaam, Lita 48,600 zinazosambazwa kwenye Halmashauri za Geita lita 8,092,Kagera lita 12,308, Kigoma lita 7,616, Lindi lita 9,048 na Mtwara lita 11,536,”amesema.

Aidha amesema lita nyingine 36,000 zimeagizwa ambapo zitasambazwa kwenye mikoa yenye mlipuko wa ugonjwa huo ikiwemo Pwani, Morogoro, Tanga na Singida.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles