22.5 C
Dar es Salaam
Friday, June 21, 2024

Contact us: [email protected]

DRC yaipongeza TPA kwa utendaji mzuri na huduma zenye ufanisi

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Mkurugenzi wa Forodha na Ushuru wa bidhaa kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo anayesimamia majimbo ya Haut Katanga, Lualaba, Tanganyika na Lomami, René Kalala Masimango na ujumbe wake umeipongeza Menejimenti ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania TPA na Wafanyakazi wake, kwa utendaji mzuri na kutoa huduma zenye ufanisi Katika Bandari zake.

Pongezi hizo wamezitoa Mei 4, mwaka huu walipotembelea Makao Makuu ya TPA na Bandari ya Dar es Salaam ili kujionea shughuli mbalimbali za kiutendaji Bandarini hapo.

“Bandari hii ya Dar es Salaam ni muhimu sana kwa mizigo inayokuja Kongo na inahudumia mizigo mingi, tumekuja kuona utendaji kazi wake na tumeona kuwa kazi ni nzuri na Bandari inamipangilio mizuri,” amesema Masimango.

Akiwakaribisha Wageni hao, Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Plasduce Mkeli Mbossa, amewashukuru kwa ziara yao na amewahakikishia kuwa Menejimenti yake ipo tayari kutatua changamoto zozote zikijitokeza katika kuhudumia Shehena ya mzigo unaoenda na kutoka Kongo kupitia Bandari za Tanzania kwa lengo la kulinda mahusiano mazuri na ya muda mrefu ya kidiplomasia na Biashara Kati ya nchi hizi mbili.

“Menejimenti ya TPA itaendelea kuzifanyia kazi changamoto zozote Katika kuhudumia Shehena ya Kongo na kuboresha mahusiano ili shughuli zinazofanywa na TPA Katika Bandari zake ziwe na manufaa kwa DRC,” alisema Mbossa.

Kwa upande wake Balozi wa Tanzania nchini DRC, Said Juma Mshana amesema ziara hiyo ni fursa ya kuwa na majadiliano ya pamoja na yenye tija kuhusu changamoto zinazoyakabili mahusiano ya kibiashara na kutafuta suluhisho kwa manufaa ya Tanzania na DRC.

“Ziara hii itasaidia kukuza mahusiano ya kiuchumi na ya kijamii pamoja na kuimarisha uchumi wa nchi hizi mbili pamoja na uchumi wa Jumuiya za Kikanda,” amesema Balozi Mshana.

Naye Balozi wa DRC nchini Tanzania, Jean Pierre Massala amesema ni ziara hii ni muhimu sana kwa mahusiano Kati ya DRC na Tanzania na muhimu ni kufanya kazi kwa pamoja kwa faida ya nchi hizi mbili.

“Ni vema kuwa na mawazo chanya katika kuimarisha Biashara kati ya DRC na Tanzania kwa faida za kiuchumi kwa nchi hizi na Watu wake,” amesema Balozi Massala.

Taifa la Kongo ni kinara kwa kupitisha kiwango kikubwa cha Shehena Katika Bandari za Tanzania hasa Bandari ya Dar es Salaam.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles