26.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Wanafunzi DMI kutembelea Korea Kusini kwa mafunzo

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Kaimu Mkuu wa Chuo cha Bahari Dar es Salaam (DMI), Dk. Tumaini Gurumo ameushukuru Ubalozi wa Korea ya Kusini kupitia Chuo Cha Korea Maritime and fisheries institute kilichopo nchini Korea kusini kwa kutoa ufadhili wa mafunzo kwa vitendo melini kwa wanafunzi wa nne (4) wa DMI.

Akizungumza jijini Dar es Salaam Mei 5, mwaka huu, Dk. Ngurumo amesema fursa hiyo ni muhimu wakati huu kwani Serikali imewekeza fedha nyingi kwenye ujenzi wa meli na uwekezaji huo utahitaji mabaharia na wahandisi wa meli wenye uzoefu ili kuendesha meli hizo hivyo kwa fursa hiyo itarahisisha uendeshaji pindi miradi hiyo itakapokamilika.

“Fursa hii imekuja wakayi muafaka kwani kwa muda huo watakaokuwepo mafunzoni watapata vitu vingi sababu wenzetu wamepiga hatua kwenye usafiri wa majini na wana meli nyingi uilinganisha na sisi,” amesema Dk.Tumaini.

Dk. Tumaini amesema pamoja na kupata fursa hiyo kwa Tanzania pia nchi itaboresha mahusiano kwenye sekta ndogo ya bahari hali itakayoleta mapinduzi makubwa wakati nchi ikiendeleea na utekelezaji wa masuala mbalimbali ya uchumi wa buluu.

Kwa upande wake Balozi wa Korea nchini, Kim Sun Pyo amesema Serikali ya Korea itaendelea kutoa nafasi kwa wanafunzi wa sekta ya bahari lengo likiwa kuwapa ujuzi wa teknolojia za kisasa ili kuwapa ujuzi katika eneo la sekta ndogo ya bahari.  

Aidha, mmoja wa wanafunzi wa DMI, Jane Mussa wameishukuru kupitia DMI kwa kuwezesha kwenda kupata mafunzo nchini Korea kwani mafunzo hayo in  moja ya matakwa ya kozi hiyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles