27.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

Mbunge Mwanga ahimiza wananchi kuweka tahadhari ya chakula

Na Safina Sarwatt, Mwanga

Wananchi wilayani Mwanga mkoani Kilimanjaro wamehimizwa kutumia vizuri akiba ya chakula kilichopo kutokana na mabadiliko ya tabianchi ambayo yamebakuwa yakiathiri uzalishaji.

Wito huo umetolewa juzi na Mbunge wa Mwanga, Joseph Tadayo wakati wa ibada maalumu ya harambee ya kuchangia ujenzi wa Kanisa la KKKT Usharika wa Lang’ata mtaa wa Kagongo.

“Kwanza niwapeni pole sana wananchi wangu wa Mwanga katika kipindi hiki ambacho taifa limekumbwa upungufu wa chakula kutokana na mabadiliko ya tabia ya nchi na kuathiri hali ya uzalishaji wa chakula.

“Mvua ilichelewa kunyesha ila kwa sasa tumepata neema ya mvua tutumie vizuri kulima mazao ya muda mfupi na ukanda wa tambalale limeni mazao ambayo yanastahimili ukame,” amesema Tadayo.

Pia ameelezea miradi ya maendeleo inayotekelezwa na Serikali jimboni humokikiwemo mradi mkubwa wa umwagiliaji Kirya, ujenzi wa Kituo cha kisasa cha Afya cha Kirya, mradi mkubwa maji Same-Mwanga-Korogwe unatarajiwa kumaliza tatizo la maji.

Sambamba na hayo, Tadayo pia aliwashukuru wabunge wenzake akiwemo Mbunge wa viti Maalumu, Shally Raymond, Dk. Charles Kimei, Esther Maleko kwa kumuunga mkono katika zoezi hilo.

Tadayo pia alishiriki harambee ya ujenzi wa msikiti wa Magulay kata ya Kirya ambao ujenzi wake uko katila hatu za uezekaji.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles