25.2 C
Dar es Salaam
Monday, April 22, 2024

Contact us: [email protected]

Drake kodi ya nyumba mil. 500/-

CALIFORNIA, Marekani

NYUMBA aliyokuwa anaishi staa wa muziki duniani, Drake, ambayo amehama hivi karibuni, haikuwa ya mchezo kwani kwa mwezi alikuwa analipa kodi ya Dola za Marekani 215,000 (takribani Sh mil. 500 za Tanzania).

Kwa mujibu wa jarida la New York Post, mzaliwa wa Canada huyo anayeishi Marekani analipa kiasi hicho kwenye mjengo wenye ukubwa wa meta za mraba zaidi ya 1672.

Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Instagram, Drake aliposti nyumba hiyo hivi karibuni wakati akisherehekea ‘birthday’ yake ya kutimiza umri wa miaka 35.

Jamaa aliishi kwenye nyumba hiyo kwa wiki chache tu kwani hakuwa na mpango wa kuishi hapo muda mrefu kwa kuwa tayari ana mjengo mwingine wa maana nje ya Jiji la Los Angeles.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles