20.9 C
Dar es Salaam
Saturday, June 15, 2024

Contact us: [email protected]

Drake ajiweka tena kwa Rihanna

BADI MCHOMOLO NA MTANDAO
BAADA ya kuwa katika uhusiano kwa muda mfupi na kisha kuachana, mwana hip hop kutoka kundi la Young Money, Aubrey Graham ‘Drake’ na msanii Rihanna wanaelezwa kurudiana upya, baada ya kuonekana maeneo mbalimbali wakifurahia umoja wao.
Miaka miwili iliyopita Drake aligombana na Chris Brown baada ya msanii huyo kuwa na uhusiano na Rihanna, wakati akijua kwamba mwanadada huyo alikuwa na uhusiano na Chris.
Ukubwa wa mgogoro huo ulifikia kipindi walirushiana chupa wakiwa klabu, lakini baada ya muda walizungumza na kumaliza ugonvi wao.
Hata hivyo, baada ya kumalizika kwa mgogoro huo bado Drake aliendelea kuwa na uhusiano wa siri na Rihanna, kupelekea Chris kuachana naye na Drake kuweka wazi uhusiano huo uliodumu kwa muda mfupi.
Mwanzoni mwa wiki hii wawili hao wamekutwa wakiingia klabu Las Vegas nchini Marekani wakiwa katika furaha na ukaribu kama wapenzi.
Hata hivyo, Drake amekanusha madai hayo, huku akidai wapo katika maandalizi ya wimbo wao mpya baada ya wa awali wa Rihanna alioupa jina ‘What’s My Name’ aliomshirikisha Drake.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles