Christian Bella: Vijana wa mtaani walinifundisha Kiswahili

0
1085

Christian-BellaNA RHOBI CHACHA
MWANAMUZIKI Christian Bella ‘King of Melody’ ameweka wazi kwamba vijana wa Kinondoni waliokuwa wakikaa katika vijiwe ndio waliomfundisha Kiswahili anachozungumza sasa.
Alisema baada ya kufika Tanzania na kugundua kwamba Kiswahili ni shida kwake, alianza kujifunza kupitia kwa vijana hao na hata baadhi ya nyimbo zake alitunga kupitia vijana hao bila wao kujua.
“Mimi nilikuwa sijui kabisa Kiswahili, yaani hata wimbo wangu wa ‘Mapenzi yako wapi’ nilitunga kupitia kwa dada mmoja aitwaye Mariam, yeye ni Mkongo, lakini anajua Kiswahili, nilikuwa sehemu nimekaa nikamwita, nikawa namuuliza neno hili nikitaka kuzungumza Kiswahili nasemaje, ananieleza mi naandika bila yeye kujua kwamba nilikuwa naandika wimbo,” alisema Bella.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here