24.1 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

DPP yaeleza sababu za kumnyima dhamana mtangazaji wa TV

NAIROBI, KENYA

WANASHERIA wa Jacque Maribe jana wamekataa jaribio la Ofisi ya Mashitaka ya Umma (DPP) kuzuia mtangazaji huyo wa Citizen TV anayeshtakiwa kwa mauaji kuendelea na kazi hiyo iwapo ataachiwa kwa dhamana.

Wakili wa Serikali, Catherine Mwaniki alitaka mtangazaji huyo azuiwe kutangaza katika televisheni kwa kile alichoeleza atawashawishi baadhi ya mashahidi wa kesi ya mauaji ya mfanyabiashara Monica Kimani.

Mwaniki alidai Maribe anapaswa kubaki rumande ili asichanganyike na umma na kuvuruga upelelezi na ushahidi.

“Tunachosisitiza siku zote ni kwamba kuwa mtangazaji maarufu wa televisheni, kuna uwezekano mkubwa wakati wa kuchangamana na umma, kutumia fursa hiyo kuwashawishi mashahidi,” alisema Mwaniki.

Maribe na mchumba wake Joseph Irungu maarufu kama Jowie wamekana kumuua Monica katika nyumba yake huko Kilimani Septemba 19, mwaka huu.

Walishtakiwa upya jana baada ya upande wa mashtaka kurekebisha hati ya mashtaka.

Mwanasheria wa Maribe, Katwa Kigen alisema mtangazaji huyo ameonesha ushirikiano usio na shaka tangu mwanzo na hivyo kustahili dhamana.

Jaji James Wakiaga alisema Maribe na mchumba wake watabakia rumande hadi Jumanne ijayo, siku ambayo mahakama itaamua maombi yao ya dhamana.

Mahakama pia itaamua iwapo mtangazaji huyo ataruhusiwa kuendelea na kazi yake iwapo ataachiwa kwa dhamana.

Wakiaga alisema anahitaji muda kupitia hoja zilizowasilishwa na upande wa mashtaka na utetezi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles