25.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

DOGO JANJA APONEA CHUPUCHUPU KUPOTEZWA

NA MWANDISHI WETU


MSANII wa Bongo Fleva, Abdulaziz  Chande ‘Dogo Janja’ amesema moja ya tukio ambalo hawezi kulisahau kwenye maisha yake ni siku ambayo yeye na washkaji zake walipokwenda kuiba kwenye ‘godauni’ kasha mwenzao mmoja akapotea.

Staa huyo wa singo ya Kidebe, ameliambia Juma3tata kuwa tukio hilo lilitokea zamani wakati anahangaika kutoka kimuziki nyumbani kwao Ngarenaro mkoani, Arusha ambapo yeye na washkaji zake walikuwa wanafanya michongo ya kukaba.

“Kuna siku tulikwenda kuiba sehemu, basi tulipofika kwenye godauni moja hivi ambalo  mara kwa mara tulikuwa tunakwenda kufanya yetu ikabidi tumtume mmoja apande juu kwenye ukuta achungulie ili kama kuna chochote tuzame tupige,

“Basi tukamsapoti jamaa wetu mmoja akapanda kwenye ukuta alipoingia ndani tukasikia tu mlio wake mmoja tu kasha kukawa kimya, hapo wote tukakimbia na siku hiyo jamaa hatukumwona sijui nini kilimkuta,” alisema Dogo Janja.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles