28.9 C
Dar es Salaam
Friday, July 19, 2024

Contact us: [email protected]

Dk.Ndumbaro aanza ziara jimboni kutatua kero za wananchi

Na Mwandishi Wetu, Songea

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo na Mbunge wa Jimbo la Songea Mjini Dk. Damas Ndumbaro ameanza rasmi ziara katika jimbo hilo kusikiliza na kutatua kero za wananchi.

Katika ziara hiyo Ndumbaro ameambatana na wataalamu mbalimbali kutoka katika Manispaa ya Songea Mjini ili kusikiliza hoja na kero mbalimbali zinazowakabili wananchi wa jimbo hilo.

Moja kati ya changamoto zilizoibuliwa katika ziara hiyo ni ukosefu wa maji wa muda mrefu katika mitaa ya kata ya Mletele ambao umetokana na kukosekana kwa bomba la kufikisha maji katika mtaa wa Mdundiko hatua iliyomfanya Ndumbaro atatue changamoto hiyo kwa kujitolea kuchangia kiasi cha Sh 500,00 ili kukamilisha kiasi kinachotakiwa ili wananchi hao wapate huduma hiyo.

Aidha Dk. Ndumbaro amewaahidi wananchi hao kutatua changamoto ya usafiri wa kufika mjini ambao umekua kikwazo katika eneo hilo.

Katika siku ya kwanza ya ziara yake amezungumza na wananchi wa Kata tatu ambazo ni kata ya Mletele, Seedfarm na Bombambili.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles