24.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Dk. Mongella akemea mapenzi ya jinsia moja

Na Nora Damian, Mtanzania Digital

Mwanasiasa mkongwe nchini, Dk. Getrude Mongella amekemea mahusiano ya jinsia moja na kutaka wanaohamasisha vitendo hivyo washughulikiwe.

Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS), Dorothea Simkwayi, akizungumza wakati wa uzinduzi wa kitabu chake kijulikanacho kama ‘Jivue ngozi ya udhaifu’.

Dk. Mongela ameyasema hayo Juni 3,2023 wakati akizindua kitabu kijulikanacho kama ‘Jivue ngozi ya udhaifu’ kilichoandikwa na Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS), Dorothea Simkwayi.

“Mimi nina watoto watatu wa kiume, nilipokwenda Marekani wakati huo haya mambo ndiyo yalikuwa yanaanza, nilikaa na wanangu nikawatahadharisha nikawaambia msije mkaniua kabla ya wakati…watoto wa kiume nataka mama zenu watembee vifua mbele.

“Nchi hii hatukuikomboa ili watu waje wafanye mazagazaga yao, haiwezekani, kama wapo waliofika hapo hilo ni gamba livuliwe,” amesema Dk. Mongela.

Aidha amewataka waandishi kuandika vitabu vitakavyolijenga taifa badala ya kuacha fursa hiyo kutumiwa na watu wengine wasioitakia mema Tanzania.

“Dorothea ametuonyesha katika umri mdogo ambao sisi wazee tumeshindwa kuandika vitabu, unatakiwa uonyeshe kile unachoweza kufanya kabla ya kusema fulani atafanya,” amesema.

Akizungumzia kitabu hicho, Dorothea amesema kinamsaidia kijana kutambua kipawa alichonacho na kukitumia vema katika kuisaidia jamii inayomzunguka.

“Wazo la kuandika kitabu nililipata tangu nikiwa kidato cha tatu, nilipitia changamoto za kiafya na nikiwa hospitali nilianza kupata mawazo ya kuandika kitabu.

“Kundi kubwa la vijana tunapitia changamoto kubwa tusipowatumia vizuri wazazi na walezi sidhani kama tutaweza kuwa na kizazi kizuri baadaye,” amesema Dorothea.

Kwa upande wake Mhariri na Mchapishaji wa kitabu hicho, Dk. Leonard Bakize, amesema kitabu hicho kinaakisi maisha aliyopitia Dorothea na kwamba kinafundisha watu kutokata tamaa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles