24.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

CHF kukutana na waajiri ili kuhamasisha wafanyakazi kujiunga na bima ya afya

Na Esther Mnyika, Mtanzania Digital

Katika kuhakikisha kila mwananchi anakuwa na uhakika wa matibabu Serikali kupitia Bima ya Taifa iliyoboreshwa (CHF) imeendelea kukutana na waajiri nchini ili kuhamasisha wafanyakazi wao kujiunga na mfuko huo.

Akizungumza leo Jumatatu Juni 6, jijini Dar es Salaam wakati wa mkutano uliowakutanisha waajiri wa viwanda na kampuni katika Manispaa ya Ubungo, Mratibu wa CHF Taifa kutoka Ofisi ya Rais Tamisemi, Silvery Maganza amesema wanampango wa kufikia sekta zote lengo likiwa kupanua mfuko huo na kuhakikisha huduma za Afya zinamfikiwa na kila mwananchi.

Amesema lengo la mfuko wa bima ya afya iliyoboreshwa ni kumfikia kila Mtanzania wa hali zote bila kujali kipato chake.

“Sasa hivi ukienda hospitali unaweza ukatumia mpaka 20,000 Kwa mara moja tu na ukiangalia hali ya maisha kwa sasa yalivyo ndiyo sababu Serikali kwa kuliona hilo imeleta huu mfuko ambao mtu mmoja analipia 40,000 anapata matibabu mwaka nzima na familia ya watu 6 ambao wategemezi wake wawe chini ya miaka 21 wanalipia Sh 150,000 na wanapata matibabu mwaka mzima bila malipo ya ziada,” amesema Maganza.

Aidha, amesema changamoto kubwa kwa sasa wananchi wengi hawana elimu ya bima na uelewa bado mdogo.

Naye, Mratibu wa CHF Wilaya ya Ubungo, Leticia Meena ametoa rai kwa viongozi na taasisi mbalimbali zilizopo wilayani hapo kushirikiana katika kutoa elimu ya bima ya afya na kushawishi wafanyakazi wao kujiunga na mfuko huo.

“Niwaombe viongozi wa sekta rasmi na zisizo rasmi kuongea na watu wao kujiunga na mfuko huu kwani utawasaidia na kuwa na uhakika wa matibabu pindi watakapougu,” amesema Meena.

Sambamba na hayo, Meena ameongeza kuwa kuna vikundi vingi vya wajasiliamali katika wilaya ya ubungo hivyo vinapaswa kuhamasishana ili kujiunga na mfuko kwa maslahi yao binafsi familia na nchi kwa ujumla.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles