23.6 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Dk. Gwajima ataka uwiano wafanyakazi sekta ya afya

Na Ramadhan Hassan, Dodoma

WAZIRI wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Dk,Doroth Gwajima amewataka waganga wakuu wa mikoa na wilaya kuendelea kutoa huduma bora kwa wateja huku akiwasisitiza umuhimu wa kuweka uwiano wa wafanyakazi wa kada ya afya katika maeneo yao kutokana na baadhi wakilundikana mijini.

Pia,amewaagiza kuhakikisha vituo vyote vya afya vilivyojengwa  na kukamilika vianze kufanya kazi kwa kutoa huduma.

Akizungumza leo Septemba 15,2021,katika mkutano mkuu wa mwaka wa kiutendaji wa waganga wakuu wa mikoa na halmashauri,Waziri Gwajima amesema ni lazima waendelee kujifunza kutoa huduma bora.

Pia, Dk. Gwajima amesema waganga hao wanatakiwa kwenda kuanza kutoa huduma katika vituo vya afya ambavyo vimekamilika lengo likiwa ni wahusika waanze kupata huduma.

“Naomba niwaelekeze vituo vya kutolea huduma za afya ambavyo vimekamilika vianze kutoa huduma,tusikubali vituo hivyo kukaa tu,ukifanya hivyo ni uzembe  unatakiwa kuwajibika twende na ‘principal’ hiyo mahitaji hayo ni mengi  tusikubali maboma kuendelea kuchakaa,”amesema.

Naye Naibu Waziri Tamisemi anayeshughulikia Afya Dk. Festo Dugange,ameiomba serikali utoaji wa chanjo ya Uviko 19 kuwa lazima kwa makundi yote maalumu huku akiwataka waganga  wakuu wa mikoa na halmashauri kuhakikisha miradi yote ya afya inakamilika kwa wakati.

Pia,amewakumbusha kusimamia rasilimali fedha zinazopelekwa katika maeneo yao ikiwa ni pamoja na thamani ya miradi ionekane.

“Kutokana na fedha za miamala tujajenga vituo vya afya katika kila jimbo, dawa na vifaa tiba kuna jitihada kubwa zimefanyika ili wananchi wawe na uhakika wa huduma za afya,”amesema.

Naye Katibu Mkuu  hiyo, Profesa Abel Makubi, amesema kuwa amekuwa akipokea malalamiko kwamba kuna baadhi ya watumishi wa afya utendaji kazi wao hauridhishi na kuwataka waganga wakuu hao kwenda kulisimamia vyema suala hilo.

Amewataka kuongeza kasi ya utendaji kazi huku wakihakikisha dawa zinapatikana katika maeneo yao na kupunguza vifo vya mama na mtoto.

Katibu Mkuu Tamisemi, Profesa Riziki Shemdoe amewaagiza waganga wakuu hao kwenda kusimamia watumishi katika maeneo yao.

Akisoma risala kwa niaba ya waganga wakuu,Dk. Japhet Simeo amesema wanakabiliwa na changamoto za upatikanaji wa dawa kutokana na Bohari Kuu ya Dawa (MSD) kuchelewa kutoa dawa licha ya baadhi ya hospitali kutoa fedha muda mrefu.

Ametolea mfano Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma ambayo imetoa fedha lakini mpaka sasa bado haijapata dawa.

Amesema wanakabiliwa na changamoto za uhaba wa watumishi hasa katika sekta ya afya na lishe ambapo ameipongeza Serikali kwa kujenga vituo vingi vya afya na vifaa tiba katika maeneo mengi nchini.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles