24.5 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Waziri mkuu awapa mwezi viongozi wa mikoa, halmashauri

Na Mwandishi Wetu

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amewapa mwezi mmoja viongozi wa mikoa na halmashauri wawe wamekutana na wafanyabiashara wadogo maarufu kama wamachinga na kupanga namna bora ya usimamizi wa shughuli za biashara ikiwamo kutenga maeneo ya kufanyia biashara zao.

Hatua hiyo ni utekelezaji wa maelekezo ya Rais Samia Suluhu Hassan aliyoyatoa jana wakati akizindua mpango wa uelimishaji na uhamasishaji wa sensa ya watu na makazi wa 2022, ambapo aliwataka wakuu wa mikoa wawe makini katika zoezi la kuwapanga wamachinga nchini na kuepuka vurugu, fujo na uonevu.

Ametoa kauli hiyo leo Jumatano Septemba 15, 2021 wakati akizungumza kwa video na Waziri, Naibu Waziri, Katibu Mkuu, Naibu Katibu wa Ofisi ya Rais-TamisemI, Waziri wa Viwanda na Biashara, Wakuu wa Mikoa, Wilaya na Uongozi wa Wamachinga.

Waziri Mkuu amewaelekeza viongozi wa halmashauri za majiji, manispaa, miji na wilaya  waone namna ya kutumia baadhi ya barabara za katikati ya majiji na miji kufungwa muda wa alasiri ili kuruhusu wamachinga kufanya biashara zao katika barabara hizo.

“Hii ni fursa nzuri kwa wajasiriamali wetu kufanya shughuli zao,”amesema Majaliwa.

Amesema viongozi hao wa mikoa kwa kushirikiana na viongozi wa machinga na machinga wanaweza kutenga maeneo maalumu na kuanzisha magulio ya mwishoni mwa wiki, utaratibu huo utawezesha wajasiriamali wengine kufanya shughuli zao za kiuchumi kama madereva wa bodaboda, na taksi watakaokuwa wakisafirisha abiria.

Kadhalika, Waziri Mkuu amewataka viongozi hao wahakikishe maeneo watakayoyatenga kwa ajili ya wamachinga kufanya biashara zao yanatambulika na yanakuwa na miundombinu muhimu kama vyoo, maji ili kuyaboresha.

Majaliwa amesema Serikali kupitia Wizara ya Viwanda na Biashara ina mkakati wa kutoa elimu kwa wajasiriamali wadogo kwa lengo la kuwapa uelewa mpana wa  biashara wanazofanya.

Naye, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-Tamisemi, Ummy Mwalimu amesema wamepokea maelekezo hayo na tayari wameshaanza kuandaa muongozo wa kuratibu shughuli za wamachinga ambao utawawezesha viongozi wa mikoa kuwasimamia wafanyabiashara hao.

Kwa upande wake, Waziri wa Viwanda na Biashara ametumia fursa hiyo kuwahakikishia wamachinga pamoja na wafanyabiashara wadogo nchini kuwa kwa sasa rasmi serikali katika sera ya Biashara Ndogo ndogo (SME) nchini imewatambua wamachinga.

Mwenyekiti wa Shirikisho la Wamachinga Tanzania, Ernest Masanja ameishukuru serikali kwa hatua inazochukua kuhusu machinga na kuahidi  kuendelea kushirikiana nayo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles