26.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

DIT yawaandaa wastaafu

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Watumishi 16 wa Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT) wanaotarajia kustaafu hivi karibuni wameaswa kuwa makini katika kuchagua miradi ya kufanya baada ya kustaafu ili kuepuka uwekezaji ambao utakuwa na changamoto kubwa kwao.

Dk. Haphsa akitoa mada kwa watumishi wa DIT wanaotarajia kustaafu.

Badala yake watumishi hao wametakiwa kujikita zaidi kwenye uwekezaji ambao hauhitaji mtaji mkubwa kwa wakati mmoja ili kuweza kupima uwekezaji huo endapo una tija.

Wito huo umetolewa leo Jumanne Agosti 31, DIT na Dk. Haphsa Hincha wa Shirika la Tija laTaifa (NIP), wakati akitoa mada inayohusu  uwekezaji mzuri baada ya kustaafu kwa watumishi 16 wa DIT wanaokaribia kustaafu.

Mafunzo hayo ya kujiandaa kustaafu na maisha baada ya kustaafu, lengo lake ni  kuwasaidia wastaafu kujua namna ya kujiandaa kustaafu, taratibu za kufuata wanapofatilia mafao yao pamoja na namna ya kujua uwekezaji unaofaa baada ya kustaafu ili waweze kuishi maisha yenye staha.

Aidha, wale ambao hawajawahi kufanya kazi ya ujasiriamali kabisa wameshauriwa kujikita zaidi katika uwekezaji ambao una viashiria kidogo vya hasara jambo ambalo litasaidia kuwapa mwanga ni wapi wawekeze zaidi ili kuepuka changamoto zinazoweza kuepukika zikiwemo za kiafya.

Waashiriki wa semina hiyo wameishukuru menejimenti ya DIT kwa kuwapatia mafunzo haya kwani yametoa  mwanga kwao kabla hawajafikia ukomo wao wa utumishi wa umma. Semina hii inaendeshwa kwa siku mbili kwa wastaafu kutoka Kampasi Kuu ya Dar es Salaaam.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles