26.6 C
Dar es Salaam
Tuesday, July 16, 2024

Contact us: [email protected]

Waziri adai uingizaji sukari kama dawa za kulevya

Na Ramadhan Hassan,Dodoma

WAZIRI wa Kilimo, Profesa Adolf Mkenda, amesema suala la uingizaji wa sukari nchini kutoka nje limejaa rushwa na kudai ni kama dawa za kulevya kwani imekuwa ikiwanufaisha watu wachache.

Akizungumza leo Jumatatu Agosti 30, jijini Dodoma wakati wa uzinduzi wa matokeo ya Sensa ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi ya mwaka 2019-2020 ulioandaliwa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS)., Waziri Mkenda amesema kutokana na hilo hatatoa kibali cha uagizaji wa sukari ya nje ya nchi kwa mtu yeyote ili kuvisaidia viwanda vya ndani viweze kuzalisha kwa wingi.

Amesema huko nyuma kuna baadhi ya mawaziri waliondolewa sababu ya sakata la utoaji wa vibali vya uingizaji wa sukari ambapo amedai Serikali ya awamu ya tano na sita imejipanga kuhakikisha inavisaidia viwanda vya ndani.

Waziri Mkenda amesema kwa sasa mwenye Mamlaka ya kutoa kibali cha uingizaji wa sukari ni Waziri wa Kilimo ambaye ni yeye hivyo hatotoa kwa mtu yeyote.

“Bunge ndio limepitisha kibali cha ukitaka kuagiza sukari lazima uwe ni mzalishaji wa sukari na mwenye uwezo wa kuzalisha tani 40,000 na hakuna ambaye ataagiza sukari mpaka kuwe na pengo,kibali kitapita kwangu na hakitapita bora niachie ngazi tunamnufaisha nani,wanaopeleka majungu wapeleke tu juzi nimefuatwa Uwanja wa ndege,hatutoi kibali ng’o,”amesema.

Hata hivyo amesema endapo sheria ya uagizaji wa sukari kutoka nje ya nchi itabadilishwa atakuwa tayari kujiuzulu kwani itakuwa imewabeba watu wenye fedha.

Kuhusiana na bei ya mafuta kuwa juu,Waziri Mkenda amesema Wizara imeweka mikakati ya kuhakikisha mbegu ya zao la alizeti inapatikana kwa wingi.

Vilevile,amesema Serikali imejipanga kuweka mikakati ya pamoja kuhakikisha mbolea inapatikana kwa wingi.

Kuhusiana na uzinduzi matokeo ya sense ya kilimo,mifugo na uvuvi ya mwaka 2019-2020,Waziri Mkenda amesema sense hiyo imewasaidia kufanya uchambuzi namna ya kufanya kilimo na ufugaji bora ambapo amedai sekta ya mazao inachangia asilimia 15 ya pato la Taifa.

Amesema wanaojishughulisha na mazao ni  ni asilimia 60 lakini katika pato la Taifa wanachangia kwa asilimia 15 ambapo amedai haki hiyo inaonesha kwamba Watanzania wanaumaskini mkubwa hasa wa maeneo ya vijijini,uwiano wa sekta za uchumi ni mbaya pamoja na tija ndogo katika sekta ya kilimo.

Kwa upande wake,Mtakwimu Mkuu wa Serikali,Dk.Albina Chuwa amesema lengo la sensa hiyo ni kutoa taarifa  katika uzalishaji wa mazao,idadi ya mifugo na ufugaji wa samaki  ambapo amedai wametumia mfumo wa kidigitali kukusanya takwimu mbalimbali.

Amesema wametumia shilingi bilioni 6 ukilinganisha na mwaka 2007-8 ambapo walitumia shilingi bilioni 10 ambapo walitumia fedha nyingi katika makaratasi.

Dk. Chuwa amesema wametumia mwezi mmoja kutangaza matokeo ya utafiti tofauti na miaka ya nyuma ambapo walikuwa wakitumia miaka miwili  hadi mitatu.

Naye,Mkuu wa Wilaya ya Dodoma,Jabir Shekimweri ameiomba Wizara ya Kilimo kufungua duka la mbegu ambalo litawasaidia wakulima kuweza kununua mbegu bora kwani wengi wamekuwa wakiuziwa mbegu feki.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles