Dimpoz aeleza alivyolizwa Marekani

0
693

DIMPOZI NA SHILOLENA CHRISTOPHER MSEKENA

MSANII Omary Nyembo ‘Ommy Dimpoz’, ameeleza namna alivyoibiwa simu yake ya mkononi akiwa nchini Marekani alikokwenda kwa ziara maalumu ya kimuziki.

Dimpoz alisema baada ya kufanya onyesho la kwanza mjini Texas aliamua kufanya ununuzi katika duka moja kubwa la nguo katika mji huo lakini baada ya muda akajikuta hana simu.

“Niliangalia mfukoni sikuikuta, nikajaribu kuipiga haikuita nilipomwambia mwenye duka akanipeleka katika kamera za usalama ndani ya duka hilo nikamuona mwizi wa simu yangu alikuwa mmoja wa wateja katika duka hilo,” alieleza Dimpoz.

Cha kusikitisha alisema simu hiyo ilikuwa na hifadhi ya nyimbo zake mpya ambazo hakutarajia kuzitoa kwa sasa na vitu vingine binafsi vingi jambo ambalo limemtia hasara kubwa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here