BSS yabaki na washiriki kumi bora

0
722

Madam-RitaNA HERIETH FAUSTINE

SHINDANO la Bongo Star Search (BSS) limefikia hatua ya kumi bora baada ya washiriki wengine wawili kuyaaga mashindano hayo.

Katika shindano hilo linalodhaminiwa na Salama Condom na kinywaji cha Coca Cola, washiriki wawili walioaga mashindano hayo jana ni Chief Agala kutokea Arusha na Amina Issa wa Mwanza.

Jaji Mkuu wa BSS, Ritha Paulsen, alisema washiriki wote wanaweza kuimba, kucheza na kumiliki jukwaa na kilichobaki kwa sasa zitawekwa namba kwenye magazeti za washiriki ili mashabiki wapige kura kuchagua mshiriki wanayemtaka awe mshindi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here