28.7 C
Dar es Salaam
Thursday, June 13, 2024

Contact us: [email protected]

DIGITALI IMERAHISISHA HUDUMA ZA AFYA, ELIMU VIJIJINI

Na Mwandishi Wetu


KONGAMANO la simu za mikononi la 360-Afrika la GSMA (Global System Mobile Association). Lililofanyika mapema mwezi huu katika ukumbi wa kimataifa wa mikutano wa Mwalimu Nyeyere jijini Dar es Salaam limeibua mambo mengi ya kimendeleo. Limeweka bayana kukua kwa kasi kwa mahitaji ya upatikanaji wa mtandao wa kidigitali Afrika kwa ujumla na hasa katika soko la ndani.

Wataalamu katika sekta ya mawasiliano wametabiri kwamba kukua kwa kasi kwa matumizi ya data yanayochochewa na kuanza kutumika kwa simu za smartphone na kuenea kwa huduma za mitandao ya kijamii.

Maoni mbalimbali yaliyotolewa katika kongamano hilo, yalionesha baya makubaliano kwamba huduma za simu za mkononi yamechangia kuongezeka kwa mahitaji ya intaneti na kupatikana kwa data yenye uwezo wa kasi. Mahitaji haya yameongezewa nguvu na juhudi za wadau mbalimbali za kutumia mtandao wa intaneti wa LTE – intaneti yenye kasi ya 4G kwa ajili ya kurahisisha maendeleo ya kijamii na kiuchumi Afrika.

“Kuongeza nguvu ya simu ya mkononi kunaboresha digitali Afrika,” Kaimu Mkurugenzi wa Tigo Tanzania, Simon Karikari alieleza manufaa ambayo wateja wanatarajiwa kupata kutokana na ukuaji huu wa haraka wa digitali Afrika.

Katika majadiliano yaliyokuwa yanaitwa, Jopo la Utabiri, Karikari alieleza kwamba kukua kwa ghafla kwa takwimu bila shaka kutaathiri mwenendo wa sasa na kubadilisha falsafa ya jamii iliyozoeleka ambayo imekuwa ndio tegemeo la utamaduni wa Afrika kulinganisha na ubinafsi wa falsafa za Ulaya.

Tathmini ya Karikari inabainisha bila shaka kwamba matumizi ya takwimu kama nyenzo ya kuendesha maboresho ambayo yataiunganisha Afrika na nchi za magharibi na kutengeza kijiji cha dunia, hatimaye kuwezesha uboreshaji na kuleta suluhisho katika mitandao ya kijamii ambayo itawezesha nchi za magharibi kufikia malengo ya masoko ya ndani.

“Manufaa ya kukua ni makubwa,” alieleza Mkurugenzi akiwa anatoa mfano wa wajasiriamali wanaochipukia kama miongoni mwa wanufaikaji wa kwanza wa maboresho yanayotarajiwa pamoja na ubia mwingine unaohusiana na teknolojia ambao utafungua njia katika maendeleo ya kijamii na kiuchumi.

Jukumu la Tigo katika kufungua maboresho ya digitali ambayo yanalenga katika kumsaidia mteja, kuishi maisha ya kidigitali.

“Tunawezesha ongezeko la smartphone na kutoa vifurushi vipya vilivyoboreshwa kama vile Halichachi, JazaUjazwe kuboresha huduma kwa wateja na kupunguza mgawanyiko wa kidigitali.”

Aliongeza: “Tuna uhakika kwamba tumejenga miundombinu ya mtandao ambao utamudu ukuaji wa mahitaji ya takwimu na kutoa huduma bora ya data kwa wateja wetu.” Kampuni imewekeza kwa kiasi kikubwa katika kuboresha mtandao na uimarishaji katika miaka mitatu iliyopita kuongeza upatikanaji wa mtandao, ambapo jambo muhimu zaidi ni ubora wa huduma za broadband ya simu.

Upatikanaji wa Broadband ya simu utasaidia jamii za vijijini kuweza kupata huduma ambazo mwanzo zilikuwa kama hazifai ikiwamo biashara kwa njia ya mtandao, afya kwa njia ya mtandao, elimu kwa njia ya mtandao na serikali kwa njia ya mtandao. Hivyo, kubadilisha namna ambavyo watu wanajifunza na wanavyofanya biashara daima, kwa mfano; Tigo inasaidia Shule Direct, Taasisi ya kijamii ambayo inatoa vifaa vya kidigitali kwa wanafunzi wa sekondari Tanzania.

Kaimu Mkurugenzi wa Tigo kwa sehemu yake ya utabiri alieleza kuwa ukuaji katika utumiaji wa teknolojia ya simu utakuja na fursa nyingi licha ya changamoto za kiuchumi na udhibiti.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles