Diamond, Zari wapata mtoto wa kike

0
1309

Diamond-Platnumz-na-ZariNA VICTORIA PATRICK (TSJ)

MKALI wa muziki wa Bongo Fleva, Naseeb Abdul (Diamond Platinum) na mpenzi wake, Zarina Hassan (Zari) wamefanikiwa kupata mtoto wa kike waliyempa jina Princess Tiffan.

“Sura ya mama yangu inatosha kueleza ni kiasi gani najisikia ndani ya moyo wangu, karibu kwenye ulimwengu Princess Tiffan” aliandika Diamond katika kurasa zake mbalimbali katika mitandao ya kijamii baada ya kumpata mtoto huyo juzi.

Baada ya kuandika hivyo, wadau na wasanii mbalimbali wa sanaa walimpongeza Diamond na Zari kwa kupata mtoto huyo. Baadhi ya waliompongeza kupitia kurasa zao mitandaoni ni Sauda Mwilima, Nisha, Queen Darlin,  Dida Shaibu, Shilole na wengine wengi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here