23.3 C
Dar es Salaam
Tuesday, May 21, 2024

Contact us: [email protected]

JK: Azam isiishie Kagame, ikashinde Afrika

PICHA KUBWA*Aipongeza kutokuwa tawi la Simba na Yanga
*Aeleza imepunguza ukame wa vikombe

NA MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete, amewatakama bingwa wapya wa michuano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati,Azam kutoishia kushinda Kombe la Kagame pekee badala yake isonge mbele na kushinda mataji makubwa ya ubingwa Afrika.
Kikwete alitoa changamoto hiyo jana Ikulu wakati alipokutana na mabingwa hao wapya wa Kagame kwa ajili ya kumkabidhi kombe hilo ambapo aliwapongeza.
Akizungumza na wachezaji wa timu hiyo, Kikwete aliwataka kuhakikisha kuwa wanaulinda ubingwa huo kwa kuhakikisha wanashinda kombe hilo la Kagame mara tatu mfululizo, ili iweze kulifanya kombe hilo mali ya klabu hiyo na Tanzania.
“Nimefurahi sana kusikia mmeshinda kombe hili, mmetutoa mchanga wa macho kwa maana Watanzania wanapenda mchezo wa soka, lakini mchezo wenyewe hauwapendi.
“Changamoto yangu kwenu ni kwamba, sasa twende zaidi ya Afrika Mashariki hapa tumefanya vizuri, tumecheza mechi zote bila kufungwa hata bao moja.

Hii safi Sasa twende mbele kwenye ubingwa wa Afrika na tucheze michuano ya ubingwa huo siyo kwa nia ya kufikia fainali bali kushinda Kombe la Ubingwa wa Afrika. Na tunaweza.

“Tuna ukame wa vikombe katika nchi yetu, kila tunaposhindwa kazi yetu imekuwa ni kutunga hadithi na maelezo ya kusingizia kwanini tumeshindwa, kazi yetu ni kutafuta watu wa kuwalaumu, mara atakuwa huyo mara yule tunatafuta mchawi tu, ifike wakati Watanzania waondokane na tabia ya kutunga hadithi na maelezo marefu na visingizio vya kushindwa kwa timu zetu katika michuano ya kimataifa,” alisema.
Rais huyo mpenda michezo, alieleza kuwa anafurahi kuona Azam imeendelea kuwa kama ilivyoanza, kwasababu moja ya mambo makubwa yanayoua timu zetu nchini ni timu kujifanya kivuli cha timu zetu kubwa Simba na Yanga, kwani ukishakuwa kivuli cha timu kubwa basi huwezi hata kuifung ahiyo timu ambayo unajifanya kivuli chake.
Hata hivyo, Kikwete alitoa rai kwa timu hiyo kuendelea na moyo wa kujituma na kufanya vizuri kwenye soka.
Azam FC ilitwaa ubingwa wa Kagame kwa kuitandika Gor Mahia ya Kenya bao 2-0 katika mchezo wa fainali wa michuano hiyo uliofanyika katika Uwanja waTaifa jijini Dar es Salaam.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles