27.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 23, 2024

Contact us: [email protected]

Diamond ndani ya BSS, wawili nje

diamondmNA MWANDISHI WETU

WASHIRIKI wawili katika shindano la Bongo Star Search (BSS), wametolewa huku wakipokea ujumbe wa kuendelea kimuziki kutoka kwa msanii wa muziki wa kizazi kipya, Nasib Abdul ‘Diamond Platinum’.

Washiriki waliotolewa jana kutokana na kura zao kutotosha ni Dorice Banyukwa na Steven Lupenza huku Frida Amani na Angelmary Kato wakifungana kwa kura na hivyo kuingizwa katika hatua ya fainali.

Diamond aliwataka washiriki hao waendeleze mafunzo waliyopewa na walimu wao wakitoka katika shindano hilo badala ya kujibweteka na kukata tamaa.

“Kama na mimi ningejihusisha na BSS leo ningekuwa mbali kimuziki, naona nyie mnao uwezo wa kufika mbali zaidi kimuziki baada ya shindano hili kuisha,” alisema Diamond.

“Naona mshindi atakayepatikana katika shindano hili atakuwa anastahili kwa kuwa wote mna vigezo vya kuwa washindi na uwezo wa kufanikisha hivyo mnao, nawaomba mtuwakilishe vema kupitia kazi yenu ya muziki,” alimaliza.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles