BAADA ya kufanya vizuri na wimbo Hallelujah miezi 11 iliyopita, staa wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz na kundi maarufu kutoka Jamaica, Morgan Heritage wapo nchini Ghana wakifanya video ya kolabo yao nyingine wakishirikiana na msanii nyota nchini humo Stone Bwoy.