23.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 16, 2024

Contact us: [email protected]

Diamond, Kiba washindwa kutamba AFRIMA

Na Mwandishi Wetu

TUZO za  muziki Afrika za AFRIMA zimetolewa usiku wa kuamkia leo nchini Nigeria, huku wasanii  wa Tanzania Nassib Abdul ‘Diamond Platnumz’  na Ali Kiba wakishindwa  kutamba katika tuzo ya msanii bora wa kiume wa Afrika Mashariki.

Tuzo  hiyo iliyokuwa inasubiriwa kwa hamu na mashabiki wa wasanii hao,   imechukuliwa na Eddy Kenzo wa Uganda.

Wasanii wengine wa Tanzania walikuwa  wanawania tuzo hizo katika vipengele tofauti ikiwamo cha msanii bora wa kike Afrika Mashariki ni Nandy, Zuchu,Rosa Ree na Spiece Diana  ambapo  mshindi wa tuzo hiyo ni Nikita Kering kutoka Kenya. 

Wengine  ni  waandaaji wa muziki Kenny na S2kizzy na Kimambo ambao nao hawakufanikiwa kuondoka na chochote, kwani tuzo ya  walikuwa katika kipengele  Producer bora wa mwaka.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles