Taarifa inasema kuwa pamoja na kuwa yuko hospitali bado mtetezi huyo mkuu wa haki za binadamu na aliyepinga utawala wa ubaguzi wa rangi nchini Afrika Kusini amepata, haijabainika ni maambukizi ya aina gani ambayo yanamsumbua.
Familia yake imesema maambukizi hayo hayahusiani na saratani ya tezi dume ambayo imekuwa ikimtatiza kwa takriban miaka 20.
Askofu Desmond Tutu, 84, amekuwa akilazwa hospitalini mara kwa mara katika miaka ya hivi karibuni na amekuwa akitibiwa maradhi ya saratani ya tezi dume.