23.3 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Aina za ukatili wanaofanyiwa watoto, wanawake – 4

Mtoto aliyefanyiwa ukatili.
Mtoto aliyefanyiwa ukatili.

Maneno yanayohusiana na ukatili wa kijinsia

WIKI iliyopita tuliangalia maneo yanayohusiana na ukatili wa kijinsia, wiki hii tunaendelea kuangalia maeneo hayo.

Jinsia: Ni neno linalotumika kuelezea mgawanyo wa majukumu kati ya wanawake na wanaume. Watu huzaliwa wakiwa wanawake au wanaume (jinsi) kujifunza kujitambua kuwa wanawake au wanaume kutokana na jinsia zao. Jinsia inatokana na tofauti katika umri, dini na utaifa, kabila na jamii. Jinsia inatokana na sababu mbalimbali kama vile umri, dini na taifa, ukabili na asili katika jamii fulani. Jinsia inatofautiana kati ya tamaduni na mila za watu, hadhi, majukumu, wajibu na nguvu iliyopo katika uhusiano baina ya watu wanaofuata tamaduni yoyote au jamii. Watu hujifunza masuala ya jamii kutokana na mwingiliano uliopo katika jamii kutokana na mabadiliko ya kijamii, kisiasa na mazingira ya utamaduni. Jinsia ina maanisha mtu kuwa mwanamke au mwanamume, mvulana au msichana katika jamii au tamaduni fulani. Jamii hufunza mweleko, tabia, majukumu, wajibu, matatizo nafasi pamoja wa wanaume na wanawake katika hali yoyote ile.

Ukatili wa kijinsia: Ni ukatili wa kijinsia unaofanywa dhidi ya mtu bila ya kupenda kwa sababu ya tofauti za kijinsia kati ya wanaume na wanawake kama inavyoelekezwa katika jamii (jinsia). Suala la GBV hapa haihusishi vitendo vya ukatili wa kingono, kimwili na tamaduni na mila potofu, uchumi na ukatili wa kijamii bali pia ukatili unaowalenga watu au vikundi kutokana na kuwa wanawake au wanaume.

Usawa wa kijinsia: Usawa wa kijinsia unamaanisha kuwa ni chanzo cha majadiliano ya kutaka wanawake na wanaume wapate haki sawa katika mgawanyo wa rasilimali mbalimbali, huduma na nafasi katika jamii. Usawa huo haumaanishi kuwa wanawake na wanaume wawe sawa isipokuwa ni lazima washiriki katika maeneo yote ya uchumi na kijamii ili kufikia maendeleo.

Kutokana na tofauti zilizopo kati ya wanawake na wanaume, usawa wa kijinsia utapatikana tu iwapo wanawake na wanaume wataonekana kuwa wako sawa. Usawa huo pia unahusisha uhusiano na mabadiliko katika taasisi na jamii ambayo inaendeleza tofauti hizo. Uwezeshaji ni mojawapo ya mikakati ya kufikia usawa wa kijinsia.

Mfumo dume: Huu ni mfumo ambao unawagawa watu katika makundi na kuwabeba wanaume ili waonekana wana uwezo wa kuamua yanayowahusu wanawake na watoto katika familia na hata katika jamii. Mfumo dume unawafanya wanaume wawe/kuwa na uamuzi unaohusu jamii au taasisi (sheria, uchumi, dini familia, utamaduni n.k) na kuwapa uwezo wa kuamua katika taasisi hizo. Mfumo dume umekuwapo tangu zamani katika familia ambao haubadiliki.

MAENEO YA UKATILI WA KIJINSIA

Ukatili wa kijinsia utaendelea kufichwa kwa sababu unaonekana kuwa kitendo cha siri ambacho mtu mwingine hastahili kukifahamu. Hata hivyo, kutokana na wanaharakati na vyombo vya habari suala la ukatili wa kijinsia kuliweka bayana inaeleka zaidi kwa watu.

Ieleweke kuwa ukatili wa kijinsia hautokei majumbani tu bali pia hutokea kwenye maeneo mengine katika jamii.

Familia: Ni moja ya sehemu ambayo nguvu iliyopo katika kaya au familia inasababisha ukatili wa kijinsia kwa kuwa ukatili katika familia na kaya hutokea majumbani na mara nyingi huonekana kama ni suala la binafsi na kufanya upatikanaji wake wa taarifa kuwa mgumu. Hata hivyo, katika miaka ya hivi karibuni kumekuwapo na jitihada za kuliweka hadharani suala la ukatili wa majumbani. Hali hi imetokana na ongezeko la utoaji wa taarifa za ukatili wa majumbani kama ilivyo katika kitabu cha Tanzania Demographic and Health Survey (TDHS, 2010. Sura ya 16-17).

Jumuiya/jamii: Kwa kukubaliana na tabia au mwenendo wa wanaume wanaofanya ukatili unaolenga katika kuwamiliki wanawake, jumuiya au jamii inakuwa ni kitovu cha ukatili wa kijinsia jumuiya au jamii ni kikundi cha watu wanaoishi pamoja wanaweza kushirikiana kijamii, kitamaduni, kidini au kikabila. Kama kikundi au jumuiya hiyo huendeleza miundo ya kifamilia iliyopo ambayo inatokana na kutokuwapo kwa usawa katika nguvu/umiliki uliopo katika jamii pamoja na mila na tamaduni potofu za kupiga na adhabu ya viboko, mahali pa kazi ikiwa ni sehemu ya jamii zinaweza pia kuwa eneo la ukatili wa kijinsia.

Aidha, huduma za serikali au biashara binafsi, wanawake wako katika hali hatarishi ya kukabiliwa na vitendo vya ukatili wa kijinsia kama vile ukatili wa kingono (unyanyasaji, ukandamizaji) na ukatili katika biashara ya ukahaba (usafishaji wa binadamu kwa ajli ya biashara ya ngono).

Itaendelea wiki ijayo…

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles