25.7 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

DENNIS AVNER: MWANAMUME ALIYEJIBADILI MWONEKANO AFANANE NA PAKA

KWA miaka mingi, Dennis Avner, ambaye kwa sasa ni marehemu alipitia mlolongo wa operesheni ili kubadili mwonekano wake ikiwamo mdomo, masikio, mashavu na paji la uso, kuchonga meno yawe makali na kuchora tattoo ili kufanikisha kuwa na mwonekano  wa Tiger jike.

Pia alikuza kucha zionekana kama makucha yale yaparurao. Pamoja na mwonekano wake huo usio wa kawaida, Avner aliendelea na kazi yake kama mtaalamu wa program za kompyuta, ijapokuwa mara nyingi alionekana katika vipindi mbalimbali vya televisheni.

Avner aliyezaliwa Agost 27, 1958 alifariki dunia Novemba 5, 2012 baada ya kukutwa akiwa amekufa nyumbani kwake, katika kile kinachoaminika kujiua kutokana na msongo wa mawazo.

Kwa michakato yake hiyo 14 ya upasuaji ili kufikia lengo hilo, anashikilia rekodi ya dunia kwa kufanyia mabadiliko mengi zaidi ya kudumu ya kumgeuza afanane na mnyama.

Anajulikana kama Stalking Cat, Paka Mnyemeleaji, jina la asili la Marekani ile nyakati za Wahindi wekundu aliliopewa wakati wa utotoni na mtaalamu wa dawa wa kabila lake.

Avner alizaliwa Flint, Michigan na wazazi wake walikuwa wa kizazi cha Lakota na Wyandot au kwa jina lingine Huron, jamii za kale za Wahindi wekundu ambao ndiyo watu wa asili ya taifa hilo. Lakini pia alizaliwa nusu mzungu na nusu Mmarekani asilia.

Alikuwa na kaka yake ajulikanaye Dave. Familia iliishi Suttons Bay, Michigan. Kama mtu mzima Stalking Cat aliwahi kueleza katika mahojiano kuwa hisia za tangu utotoni za kutaka kufanana na mnyama huyo alikuwa bado anazo.

Anakumbuka akiwa mdogo jinsi alivyokuwa akijiuliza maswali kama vile wapi ulipo mkia wake!. Katika umri wa miaka 10, akapewa jina la Stalking Cat na Grey Cloud, mtaalamu wa dawa wa kabila lake.

Aidha katika mahojiano mengine, Stalking Cat alieleza kuwa wakati wa utoto wake marafiki zake walikuwa watu wazima. Hakuhusiana na watoto wa umri wake, na alitumia sehemu kubwa akiwa porini.

Aidha alifichua kuwa hakumfahamu baba yake na alidai kuwa baba wake wa kambo alikuwa mdhalilishaji watoto. Wakati alipoulizwa iwapo alikuwa mwathirika wa vitendo hivyo vichafu vya babake wa kambo, Cat alijibu, “Si kwa kiwango hicho, lakini imetosha. Namaanisha, nimepata matatizo ya kisaikolojia, ambayo kamwe hayataondoka.

Stalking Cat alihitimu kutoka Shule ya Juu ya Oscoda mwaka 1977. Kama  mtu mzima akajiunga na jeshi la majini kama mtaalamu wa mawimbi ya majini. Hata hivyo, akaacha kazi jeshini mwaka 1981 na kuanza kufanya kazi kama mtaalamu wa program za kompyuta huko San Diego, California.

Mapema miaka ya 1980 akaanza kujibadili usoni kabla ya kuhamia maeneo mengine ya mwili.

Katika moja ya mahojiano alisema kuwa alichagua kubadili mwonekano wake kwa mujibu wa utamaduni wa kale wa jamii yake ya Wyandot, ambayo watu walibadili miili kufanana na alama (miungu) yao, ikimaanisha kwa upande wake mnyama wa jamii ya Paka hasa Tiger alikuwa nembo, alama na mungu wake.

Alieleza kuwa alikutana chifu wa Mmarekani wa asili ambaye alimtia moyo kufuata njia ya mungu wake, tiger. Pia alimwambia namna nembo yake hiyo ni Tiger wa kike. Mwaka 2005 akiwa na umri wa miaka 47 akahamia Washington kuungana na mmoja wa marafiki zake waliohamia huko kutokana na sababu za mkataba na kampuni ya utengenezaji ndege ya Boeing.

Rafikiye huyo Calhoun na mumewe mhandisi wa ndege Rick Weiss walihamia Freeland, Washington, Kisiwa Whidbey, ambako Stalking Cat alisaidia kuiweka sawa nyumba yao, akaishi nao.

Magazeti ya eneo hilo yakaanza kummulika mara kwa mara yakimuandika makala. Lakini Stalking Cat akaingia katika matatizo ya kifedha na Agosti 2007, aliweka ujumbe katika jarida la mtandoani akisema anatafuta mahali pengine pa kuishi.

Calhoun aliweka ujumbe akisema yeye na mumewe hawakuwa na uwezo tena wa kuweza kumsaidia na kwamba watamfanyia sherehe kuba ya kumuaga.

Septemba 2007, akiwa na umri wa miaka 49, Stalking Cat akahamia  Tonopah, Nevada na  Novemba 5, 2012, akafariki dunia akiwa peke yake katika gereji akiwa na umri wa miaka 54. Taarifa za kifo chake zikawa hadharani wiki moja baadaye. Inaaminika alijiua. Inasemekana alikuwa ametopea katika ulevi na dawa za kulevya.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles