24.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

DC KIBAHA KUFUTA HATI ZA VIWANJA 1,000

NA GUSTAPHU HAULE -PWANI

MKUU wa Wilaya ya Kibaha mkoani Pwani,  Asumpter Mshama, ametangaza kufuta hati za viwanja 1078 vilivyokuwa vinamilikiwa na taasisi za umma   na makampuni mbalimbali kutokana na kushindwa kuviendeleza.

Vilevile  ametoa muda hadi kufikia Agosti 31, mwaka kuhakikisha wamiliki wa viwanja hivyo wanajitokeza haraka na kusaini makubaliano ya kuviendeleza haraka.

Akizungumza na waandishi wa habari  mjini hapa juzi, alisema amefikia hatua hiyo baada ya kuona mapori yamekuwa makubwa na wenye viwanja hivyo wameshindwa kuendeleza jambo ambalo linachangia kuwapo vichaka vya mauaji.

Alisema kati ya hivyo viwanja 735 vipo katika Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha Vijijini huku katika Halmashauri ya Kibaha Mjini ikiwa na viwanja 343 na kwamba vilipimwa na wahusika kupewa hati za kumiliki lakini hadi sasa hawajaviendeleza.

Mkuu huyo wa wilaya alizitaja baadhi ya taasisi na kampuni ambazo zinatarajiwa kufutiwa hati hizo ni Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Shirika la Ugavi wa Umeme(Tanesco), Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru),  Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (Open)   na Njuweni hotel.

“Hizi taasisi na makampuni mengine ambayo hayajatajwa yalipewa umiliki wa viwanja miaka mingi lakini wameshindwa kuviendeleza.

“Matokeo yake Kibaha imebaki kuwa kichaka cha watu kuuwana hivyo kwa sasa hatutaangalia taasisi wala kitu chochote vyote vinafutwa,” alisema Mshama.

Alisema   alitoa tamko mwaka jana la kuwataka wamiliki hao waviendeleze viwanja vyao lakini wamekaidi agizo na mpaka sasa hakuna aliyefanya chochote hivyo hakuna huruma tena kinachofuata ni utekelezaji.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles