31.7 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

DC Geita ajitetea mbele ya wabunge EALA  

herman-kapufiNa BENJAMIN MASESE-GEITA

MKUU wa Wilaya ya Geita mkoani Geita, Herman Kapufi, amesema ofisi yake haitakuwa miongoni mwa taasisi za umma zinazodaiwa ankara za maji na umeme kwani kitendo hicho ni sehemu ya kukwamisha na kurudisha maendeleo nyuma.

Kauli hiyo aliitoa jana baada ya  wabunge wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki (EALA) chini ya Kamati ya Hesabu walipomtembelea  ofisini kwake ili kupata  maelezo juu ya miradi ya maji inayotekelezwa wilayani humo kwa ufadhili wa  fedha kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB).

Kapufi alilazimika kujitetea hivyo baada ya kuulizwa na wabunge hao kwamba ni mkakati gani alionao wa kuhakikisha ofisi za umma zilizo chini yake zinalipa ankara za maji na umeme kwa kuwa zimekuwa sehemu ya kukwamisha miradi kutokana na kuwa wadaiwa sugu huku zikitumia maji mengi.

Kapufi alisema Rais Dk. Magufuli amempa heshima kubwa ya kuwa mkuu wa wilaya iliyopo Mkoa wa Geita, hivyo atahakikisha kila idara inalipa ankara za maji ili kuwa mfano.

“Ni kweli ofisi nyingi za umma zimekuwa zikidaiwa madeni yatokanayo na huduma ya maji na umeme lakini hadi sasa ofisi yangu haidaiwi hata senti tano, kama DC lazima niwe mfano maana nimepewa heshima kubwa na rais wangu.

“Kuna watu wanatumia mgongo wa Serikali kutolipa, binafsi nawahakikishieni nitakuwa mstari wa mbele kuhamasisha wananchi na idara zangu kulipa ankara za maji ili miradi hii iliyofadhiliwa na AfDB iweze kuondoa tatizo la maji,” alisema.

Kwa upande wa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita, Modest Polinary, aliwaeleza wabunge wa EALA sababu ya miradi ya maji ya Kagera, Mbugani na Usindakwe kutekelezwa kwa asilimia 55 tofauti na miradi mingine iliyofikia asilimia 100 kwamba ni kutokana na wananchi kukatalia maeneo yao kupitisha miundombinu ikiwamo mabomba.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles