30.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

DC Buhingwe na Viongozi REA wajadili Miradi ya Umeme vijijini

Na Veronica Simba, Kigoma

Mwenyekiti wa Bodi ya Nishati Vijijini (REB), Wakili Julius Kalolo na Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi Hassan Saidy, wamemtembelea Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe, Kanali Michael Ngayalina na kujadiliana kuhusu utekelezwaji miradi ya umeme vijijini, wilayani humo.

Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe, Kanali Michael Ngayalina (kulia) akiagana na Mwenyekiti wa Bodi ya Nishati Vijijini (REB) Wakili Julius Kalolo, baada ya kikao baina yao kujadili kuhusu utekelezwaji wa miradi ya umeme vijijini wilayani humo. Wakili Kalolo alifuatana na Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA) Mhandisi Hassan Saidy (hayupo pichani), wakiwa katika ziara ya kazi Desemba 22, 2021.

Viongozi hao wamejadili kuhusu ufanisi, changamoto za miradi na namna ya kuzitatua kwa lengo la kufanikisha azma ya Serikali katika kuhakikisha wananchi wote waishio vijijini wanafikishiwa nishati ya umeme awamu kwa awamu.

Kikao hicho kilichofanyika ofisini kwa Mkuu wa Wilaya, Desemba 22, 2021 kiliwashirikisha pia wataalam kutoka REA, TANESCO pamoja na Mkandarasi Kampuni ya M/s CCCE Etern Consortium ya nchini China, inayotekeleza Mradi wa Umeme Vijijini, Awamu ya Tatu, Mzunguko wa Kwanza wilayani humo.

Akiwasilisha taarifa mbele ya Mkuu wa Wilaya, Mwakilishi wa Msimamizi wa Miradi ya REA Kanda ya Magharibi, Mhandisi Evance Kabingo alieleza kuwa Wakala hiyo imeendelea kutekeleza miradi ya umeme vijijini wilayani humo kwa ufanisi ambapo kupitia Mradi wa REA Awamu ya Tatu Mzunguko wa Kwanza, jumla ya vijiji 22 vimepelekewa umeme, mashine umba 70 zimefungwa na wateja wa awali 2,496. wameunganishiwa umeme

Akizungumzia kuhusu wananchi wote kufikiwa na huduma ya umeme, Mkurugenzi Mkuu alisema azma hiyo ya Serikali itatimizwa hatua kwa hatua kupitia miradi mbalimbali hivyo hakuna haja kwa mtu yeyote kuwa na hofu kuwa hatofikiwa.

Akieleza zaidi, Mhandisi Saidy alifafanua kuwa hatua ya kwanza inayoendelea kutekelezwa ni kuhakikisha miundombinu ya umeme inafika katika kila kijiji na kuunga wateja wa awali, kisha miundombinu hiyo itatumika katika kusambaza umeme kwa wakazi wote wa eneo husika, awamu kwa awamu.

“Nafahamu kuwa wapo wanaodhani kuwa wamerukwa na kwamba hawatafikiwa na umeme baada ya kuona miundombinu imefika katika vijiji vyao lakini wao hawajaunganishiwa. Niwatoe hofu kuwa wote watafikiwa hatua kwa hatua kupitia miradi mbalimbali inayoendelea kutekelezwa,” alifafanua.

Kuhusu changamoto katika utekelezaji wa miradi husika, Mwenyekiti wa Bodi alimweleza Mkuu wa Wilaya kuwa ni pamoja.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles