30.2 C
Dar es Salaam
Monday, November 18, 2024

Contact us: [email protected]

DC AWAPA SIKU SABA WACHIMBA KOKOTO

NA CHRISTINA GAULUHANGA-DAR ES SALAAM


MKUU wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi, ametoa siku saba kwa wachimba kokoto wa eneo la Boko Chama kuondosha mawe yao yaliyopo kwenye eneo hilo, ili kupisha ujenzi wa dampo la kisasa.

Hapi alitoa kauli hiyo baada ya kutembelea na kukagua eneo hilo ambalo awali wachimbaji wake walipewa amri ya kutokuendelea na uchimbaji wa kokoto ambapo baadhi wamekaidi amri hiyo na kuendelea.

Hapi aliwataka wachimbaji hao kutokuendelea kuchimba na hasa katika kipindi hiki cha mvua kwani wanaweza kujisababishia madhara ya kufukiwa na kifusi na kupoteza maisha.

“Maofisa mazingira na mipango miji wa manispaa undeni timu  ili mwangalie uwezekano wa kuweka dampo kwenye eneo hili kwani eneo la dampo lililopo ni moja la Pugu Kinyamwezi ni mbali,” alisema Hapi.

Mkuu huyo wa wiaya alisema dampo hilo lifanywe la kisasa ili uwe mradi ambao utasaidia kuingiza mapato kwa manispaa.

Aliongeza kuwa eneo hilo litakapoanza kutengenezwa watu waliokuwa wakichimba hapo waandae orodha ya majina ili mawe yatakayotolewa wapewe wao.

Kwa upande wake Ofisa Mazingira wa wilaya hiyo, Mohamed Msangi, alisema eneo hilo likifanywa dampo litarahisisha utupaji taka kwa wakazi wa eneo la Boko, Mabwepande, Bunju, Kawe na Mwenge.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles