24.4 C
Dar es Salaam
Wednesday, June 19, 2024

Contact us: [email protected]

DC awachachamalia wavuvi haramu Ziwa Nyasa

GUSTAPHU HAULE-RUVUMA

MKUU wa Wilaya ya Nyasa, Mkoa wa Ruvuma, Isabella Chilumba, amewapiga marufuku wavuvi wanaotumia nyavu haramu katika Ziwa Nyasa.

Amesema kwamba, mvuvi yeyote atakayekamatwa akiwa na nyavu haramu, hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yake ikiwa ni pamoja na kuteketeza vifaa vyake vya uvuvi pamoja na kupelekwa mahakamani ili sheria ifuate mkondo wake.

Chilumba alitoa kauli hiyo juzi katika Kijiji cha Mbambabay kilichopo wilayani hapa, baada ya kukamilisha zoezi la kuteketeza nyavu haramu zilizokuwa zikitumiwa na wavuvi katika ziwa hilo.

“Leo tumeteketeza nyavu haramu 115 na mitumbwi 122, vyote vikiwa na thamani zaidi ya Sh milioni 29.

“Operesheni hii itakuwa endelevu, kwa hiyo nawaomba wavuvi wote wanaotumia Ziwa Nyasa, wabadilike kwa kutumia nyavu zenye viwango vinavyokubaliwa na Serikali.

“Uteketezaji wa nyavu haramu katika ziwa hilo ni oparesheni maalumu ambayo itakuwa endelevu ili kuhakikisha tunatoa elimu kwa wavuvi juu ya athari za kutumia uvuvi haramu unaoendana na matumizi ya nyavu haramu na vifaa vyingine.

“Kwa ujumla, Serikali haikubaliani na uvuvi haramu kwa kuwa jambo hilo linaleta athari kubwa ikiwamo kuharibu mbegu za samaki wadogo ambao ni tegemeo la baadaye,” alisema Chilumba.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Nyasa, Jimson Mhagama, alisema Serikali inapiga vita uvuvi haramu kwa kuvisaidia vizazi vijavyo ili viweze kunufaika na rasilimali zilizopo katika Ziwa Nyasa hususani samaki. “Serikali kama ikikaa kimya, vizazi vijavyo vitakuwa vimekosa haki ya kutumia rasilimali zilizopo katika ziwa letu hili na ili kufikia malengo hayo, ni vema wananchi, wavuvi na Serikali wakashirikiana kwa pamoja kupiga vita

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles