28.3 C
Dar es Salaam
Wednesday, February 21, 2024

Contact us: [email protected]

DC atoboa siri wasichana kutopata wachumba

Na BENJAMIN MASESE-MWANZA

MKUU wa Wilaya ya Nyamagana, Dk. Philis Nyimbi amewataka wanawake nchini kumuomba Mungu ili kujifungua watoto wa kiume  kwa lengo la kuleta uwiano utakaosaidia watoto wa kike kuolewa  kwa urahisi tofauti na ilivyo sasa.

Kauli hiyo aliitoa juzi  kwa nyakati tofauti katika  mikutano ya ziara yake ya kutembelea kata 18 za Jiji la Mwanza kusikiliza na kutatua kero zinazowakabili wananchi huku akiwa ameambatana na idara mbalimbali zikiwamo Tanesco, Tarura, Nida, Mwauwasa, polisi na nyinginezo.

Akiwa Kata ya Mahinda Mtaa wa Igelegele, alisema hivi sasa wanawake wengi  waliofikisha umri wa kuolewa wameshindwa kupata wachumba wa kuwaoa pale wanapofikisha umri kutokana na wanaume kuwa wachache jambo ambalo kwa 

namna moja au nyingine linawaathiri wanawake.

Dk. Nyimbi alisema  kutokana na hali hiyo wanawake nchini wanatakiwa kumuomba Mungu na kuwatumia watalaamu wa afya ili kujifungua watoto wa kiume wengi ambao huko mbeleni wataweza kupata wachumba.

“Ni jambo ambalo si kificho kwamba hivi sasa wanawake tunapata shida sana mitaani, tumekuwa wengi kuliko wanaume na tunapofikisha umri wa kuolewa hatupati wachumba badala yake tunabaki kuhangaika mitaani, ni kweli si kweli,” aliwahoji wanawake na kuitikia kweli.

“Sasa naomba masuala ya kufuata nyota ya kijani achaneni nayo hata kama ukifika kituoni na kupewa elimu na mtaalamu 

“Rais wetu Dk. John Magufuli amesema tuzae na mimi binafsi namuunga mkono kwa sababu ardhi bado tunayo, isitoshe watoto wetu wanasoma bure , madarasa katika shule zetu yamejengwa kwa hiyo hakuna wasiwasi, jambo la muhimu ambalo sisi  wanawake tunapaswa kuliangalia ni kuzaa watoto wa kike vinginevyo tutaendelea kukosa wanaume wa kutuoa.

“Hebu tuangalia katika mkutano huu wa leo ni wa akina nani  wapi wengi hapa wanawake au wanaume?” alihoji huku  umati wa wanawake wakiitikia 

“Naomba tukifika katika nyumba zetu tufanye kweli lakini tukiwa tunamuomba Mungu, pia tutumie ushauri wa watalaamu wa afya,”alisema.

Katika hatua nyingine aliwapongeza wanawake kwa namna wanavyojituma katika ujasiriamali ambapo aliwataka kuunda vikundi ili kupata asilimia mbili ya kila kundi ambazo zinatolewa na Halmashauri ya Jiji la Mwanza.

Kuhusu kero alisema  asilimia kubwa zilizowasilishwa na wananchi wa Kata ya Mahina ni migogoro ya ardhi, ukosefu wa maji ya uhakika, umeme na ubovu wa miundombinu ya barabara.

Kutokana na hilo Dk. Nyimbi aliwaagiza maofisa wa Serikali aliombatana nao kutatua kero hizo ndani ya wiki moja na kumpelekea mrejesho ofisini kwake.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles