28.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

SIMBA BABA LAO

NA SOSTHNES NYON-DAR ES SALAAM

SIMBA imerejea kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, baada ya jana kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Ruvu Shooting, katika mchezo  uliochezwa Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Kwa ushindi huo, Simba ambayo juzi iliteremshwa hadi nafasi ya pili na Kagera Sugar iliyokamata usukani, baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Lipuli, imefikisha pointi 25 na kukamata uongozi wa ligi hiyo.

Mabao ya Simba katika mchezo huo yalifungwa na Miraj Athuman,  aliyefunga mawili dakika za 39 na 74 na jingine lililowekwa kimiani na Gerson Fraga dakika ya 47.

Miraj alifunga bao la kwanza kwa kichwa, baada ya kuunganisha krosi makini ya beki Shomari Kapombe kutoka upande wa kulia,huku jingine jingine akifunga kwa shuti.

Fraga kwa upande wake alipachika bao kwa shuti baada ya kutokea kashikashi langoni mwa Ruvu Shooting, iliyotokana na kona iliyochongwa na kiungo Fransis Kahata.

Kwa ujumla kipindi cha kwanza, Simba ndio iliyofanya mashambulizi mengi langoni mwa wapinzani wao Ruvu Shooting, ambapo Miraj na mshambuliaji Meddie Kagere walionekana kuwa na uchu wa kufunga.

Miraj sasa amefikisha mabao sita msimu huu akiwa na jezi ya Simba, huku akimwacha Kagere akiongoza chati  ya ufungaji akiwa na mabao nane, licha ya jana kushindwa kutikisha nyavu za Ruvu Shooting.

Kipindi cha pili, kila upande ulifanya mabadiliko kwa lengo la kusaka mabao, Simba ikitaka kuongeza na Ruvu Shooting kusawazisha.

Simba ndiyo iliyonufanika na mabadiliko iliyofanya baada ya Miraj na Fraga kila mmoja kupachika bao moja na kuwafanya Wekundu hao wa Msimbazi kukamilisha dakika 90 za kutakata kwa ushindi wa mabao 3-0.

Katika mchezo huo, Shaaban Msala na Zuberi Dabi wa Ruvu Shooting walilimwa kadi za njano kutokana na mchezo usio wa kiungwana.

Kikosi Simba;Aishi Manula, Shomari Kapombe, Mohamed Hussein, Tairone Santos, Pascal Wawa,Gerson Fraga, Hassan Dilunga/Deo Kanda DK 64, Mzamiru Yassin, Medie Kagere/Ibrahm Ajib Dk76, Miraj Athuman, Fransis Kahata.

Kikosi Ruvu Shooting; Ruvu Shooting Mohamed Makala,Omary Kindamba,Kassim Simbaulalanga,Renatus Ambro, Rajab Zahir, Zuber Dabi, Emmanuel Martin, Shaban Msala/Mosses Shabaan, Sadat Mohamed, Said Dilunga/Fullyzuzu Maganga, na  Edward Christopher/Abdulhaman Musa.   

Katika michezo mingine ya ligi hiyo Mtibwa Sugar iliilazimisha suluhu Biashara Mara Uwanja wa Karume mjini Musoma, Singida United ikaibuka na ushindi wa  bao 1-0 ugenini dhidi ya Mbeya City Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya, wakati Azam ikanoga kwa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Mbao FC iliyokuwa nyumbani Uwanja wa CCM Kirumbe, Mwanza.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles