26.3 C
Dar es Salaam
Thursday, November 28, 2024

Contact us: [email protected]

DC APIGA ‘STOP’ UPIKAJI CHAKULA KANDO MWA BARABARA

Na JOSEPH LINO-DAR ES SALAAM


MKUU wa Wilaya wa Ilala, Sophia Mjema, amepiga marufuku upikaji wa chakula kandokando mwa barabara zilizo eneo la Kariakoo, jijini Dar es Salaam.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mpango wa usafi wa magari ya kisasa na ‘dustbin’ wa kampuni ya Green Waste Pro Ltd alisema barabara zimekuwa zikiharibika kutokana na watu kupika vyakula kado mwa barabara.

“Napiga marufuku wanawake na wanaume kupika vyakula barabarani kuanzia sasa na kama wanataka kupika wapike nyumbani kwao walete vyakula kwenye ‘hotpoti’,” alisema Mjema.

Alisema kama watu wanataka kuanzisha migahawa waende Manispaa wakapewa eneo maalumu la kupikia chakula.

“Nimeagiza wasimamizi wa usafii wahakikishe hakuna mahali watu wanapika pembeni mwa barabara zetu na atakaekaidi achukuliwe hatua,” alisema.

Katika mpango huo wa usafi Green Waste Pro, yalizinduliwa magari manne ya kisasa na takataka yanayotumika kuifadhi uchafu katika manispaa hiyo.

Meneja wa Green Waste Pro Ltd, Abdallah Mbena alisema magari hayo yatasambazwa katika kata tatu za wilaya hiyo.

“Pia tumeongeza gari la kisasa la kufagia na kupiga deki barabani pamoja na magari matatu ya kusombea takataka,” alisema Mbena.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles