25.2 C
Dar es Salaam
Monday, November 25, 2024

Contact us: [email protected]

DC AMCHARAZA MZAZI WA WATOTO WALIOVUNJA KIOO CHA GARI LAKE

 

Na RAMADHAN HASSAN

MKUU wa Wilaya ya Chemba, Simon Odunga  amemcharaza viboko mzazi wa watoto walioshambulia gari lake kwa kuvunja kioo kwa jiwe.

Tukio hilo lilitokea jana katika barabara ya Kondoa-Dodoma kwenye kijiji cha Paranga wilayani Chemba wakati Mkuu huyo wa Wilaya akipita na gari lake lenye namba za usajili STL 669.

Watu walioshuhudia tukio hilo waliliambia MTANZANIA Jumamosi kuwa; Watoto hao walilirushia mawe gari hilo na hivyo kuvunja kioo cha nyuma hali iliyomlazimu Mkuu huyo wa Wilaya kuwakimbiza lakini hakuweza kuwakamata.

Kwa mujibu wa mashuhuda hao, baada ya kushindwa kuwakamata Mkuu huyo wa Wilaya aliulizia majirani waliokuwepo eneo na kumwambia kuwa ni wa Shindika Majala.

Odunga akiongozana na majirani hao alilazimika kwenda nyumbani kwa watoto hao ambako alikutana na Mzazi wao.

Mashuhuda hao wanasema kuwa Mkuu huyo wa Wilaya, Odunga alipomueleza mzazi huyo juu ya tatizo lililomkuta alimjibu kwa jeuri huku akisisitiza kuwa aliyevunja kioo si mtoto wake na wala hawezi kwenda popote.

“Aliyevunja kioo ni mtoto…chukueni tu hatua yoyote haki yangu mtaipata”.

“Malezi malezi gani mtoto ametoka shule mi nitajuaje mi najua yupo shule sijui kama amevunja kioo,”alisema Mzazi.

Ni majibu kama hayo ndiyo yaliyoonekana kumkera Odunga ambaye alianza kumcharaza viboko mzazi huyo.

Inaelezwa kuwa hatua hiyo ilimlazimisha Mwenyekiti wa kitongoji ambaye jina lake hatukuweza kulipata mara moja kuingilia kati.

Mwenyekiti huyo alikiri kuwapo kwa  matukio hayo ya kurushia mawe magari katika eneo hilo na kwama walikwishayakemea katika mkutano wa kitongoji na yalipungua.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti huyo wanaofanya matukio hayo ni watoto na vijana wa eneo hilo.

Akizungumzia na tukio hilo, Odunga alisema kijiji hicho kimekuwa na tabia hiyo ya kuweka mawe barabarani pamoja na kupiga magari mawe jambo ambalo si sahihi.

Alisema wanajipanga kwa ajili ya kuanza operesheni ya kuhakikisha tabia hiyo inakomeshwa,kwa sababu ni hatari kwa wasafiri na jamii kwa ujumla.
Alisema kwa kushirikiana na polisi wataendelea na msako ili kubaini familia ambazo zina vijana wenye tabia hiyo hususani ya Majala ambayo jamii inayowazunguka imewanyooshea kidole.Kutokana na tukio hilo, gari la polisi lilitinga katika eneo hilo na kuwachukua watu sita wakiwahusisha na tukio hilo.

- Advertisement -

Related Articles

1 COMMENT

  1. Kuu kakosea . Hata uwe mkuu wa Wilaya fuata sheria za nchi. Huruhusiwa kupiga watu. Aliyevunja ni mtoto, unampigaje mzazi tena mbele ya hadhara. Je hii ndiyo sheria ya Tanzania. Haupo juu ya sheria inabidi ufungwe wewe na ushtakiwe, pia usiwe mkuu wa mkoa tena. Mpelekeni mahakamani na amlipe mzazi .Hawa ni viongozi walioteuliwa na raisi na hawana sifa. Kiongozi yeyote kuchukua fimbo hadharani kumpiga mzazi, ilibidi huyu kiongozi ashambuliwe kwa kuleta fujo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles